Kiboguru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kiboguru ni lugha ya Kibantu nchini Sudan Kusini inayozungumzwa na Waguru. Idadi ya Waguru nchini Sudan Kusini imehesabiwa kuwa watu 500 tu lakini wote wamebadili kutumia lugha ya Kizande badala ya lugha yao ya Kiboguru, maana yake lugha ya Kiboguru haina wasemaji tena. Pia kuna Waguru nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwa wakimbizi kutoka nchini Sudan Kusini. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiboguru iko katika kundi la D30.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiboguru kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.