Khan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Khan ((可汗 - Kichina: kèhán; kwa maandishi ya Kiarabu: خان‎) ni cheo cha mtawala chenye asili kati ya wafugaji Wamongolia na Waturki wa Asia ya Kati. Mwanzoni kilikuwa cheo cha kijeshi kilichomaanisha Mkuu, amirijeshi au Bwana mkubwa. Baadaye ilimaanisha hasa mtawala. Kiasili cheo kilikuwa "khagan" lililofupishwa kuwa "khan" pekee.

Wamongolia waliongozwa na Chingis Khan na kutokana na sifa zake matumizi ya cheo hiki kilisambaa pande nyingi za Asia.

Madola mengi yaliyoongozwa na wasemaji wa Lugha za Kiturki yalitawaliwa na makhan au makhagan. Baadaye cheo hiki kilitumiwa pia kwa makabaila wa ngai za chbini zaidi.

Leo hii "Khan" anayejulikana hasa ni Aga Khan ambaye ni kiongozi wa kidini wa Waislamu akitazamiwa kama Imam wa Nizari katika jumuiya ya Waismaili. Imamu wa 46 alipewa cheo hiki kama heshima na Shah wa Uajemi wakati wa karne ya 19. Wafuasi wake wameendelea kutumia cheo hiki hadi leo.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]