Nenda kwa yaliyomo

Kevin Hassett

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
picha ya kevin Hassett (2018)

Kevin Allen Hassett (amezaliwa 20 Machi 1962) ni mchumi wa Marekani ambaye alikuwa Mshauri Mkuu wa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Washauri wa Kiuchumi katika utawala wa Donald Trump kutoka mwaka 2017 hadi 2019.

Ameandika vitabu kadhaa kikiwemo Dow 36,000, kiliyochapishwa mnamo 1999, ambacho kilielezea kwamba soko la hisa lilikuwa juu. Muda mfupi baadaye, dot-com bubble ilipasuka, na kusababisha kushuka kwa bei ya soko la hisa.

Hassett amefanya kazi katika Taasisi ya Biashara ya Amerika.[1]Alikuwa mshauri mkuu wa uchumi katika mchujo wa urais wa Chama cha Republican cha Amerika, na pia mshauri wa uchumi wa mwaka 2004 katika uchaguzi wa rais wa Amerika mnamo mwaka 2004 katika kampeni ya George W. Bush na mwaka 2008 katika kampeni ya McCain. Alikuwa tena mshauri wa uchumi katika Kampeni ya urais mnamo mwaka 2012.[2]

Katika utawala wa Trump, Hassett alikuwa Mwenyekiti wa 29 wa Baraza la Washauri wa Kiuchumi kutoka Septemba 2017 hadi Juni 2019.[3][4][5]

Maerejeo

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Trump picks conservative think tanker to chair Council of Economic Advisers", CNBC, February 24, 2017. 
  2. "Who Are Obama's and Romney's Key Economic Advisers?". nationaljournal.com.
  3. Michelle Jamrisko (Aprili 7, 2017). "Trump Names Hassett to Head Council of Economic Advisers". Bloomberg News. Iliwekwa mnamo Aprili 9, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Long, Heather (Aprili 10, 2017). "Meet Trump's newest economic adviser: Kevin Hassett". CNNMoney. Iliwekwa mnamo Aprili 11, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Roll call vote PN457", United States Senate, September 12, 2017. 
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kevin Hassett kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.