Nenda kwa yaliyomo

Kenya African Union

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya KAU,mwaka 1951

Kenya African Union (KAU) (awali Kenya African Study Union) ilikuwa shirika la siasa liliyoundwa mwaka wa 1944 [1] kwa kueneza malalamiko ya wananchi wa Kenya dhidi ya utawala wa kikoloni wa Uingereza wa wakati huo. Shirika la KAU ilidai haki za kuingia mashamba ya Kenya Highlands, ambayo hadi wakati huo, yalikuwa yakimilikiwa sanasana na wakoloni. [1] KAU walijaribu kueneza umoja kwa kuepuka siasa za kikabila zaidi ya waliyetangulia, Kikuyu Central Association.

Mwisho wa mwaka 1946, Kenyatta alirudi Kenya akiwa mwongozi[1] asiyepingwa katika harakati za kinchi. Kati ya 1947, Jomo Kenyatta alichaguliwa kuwa rais wa Kenya African Union.

Katika 1960, KAU, Kenya Independent Movement na Chama cha People's Congress waliungana kuunda Kenya African National Union (KANU).

KAU hujadliwa kwa sura moja ya kitabu cha Weep Not, Child , kilichoandikwa na Ngugi wa Thiongo

  1. 1.0 1.1 1.2 [0] ^ "Kenya - History", East Africa Living Encyclopedia (ona: Viungo vya nje).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]