Nenda kwa yaliyomo

Kemia kichambuzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Upimaji kwa moto unaonyesha kuwepo kwa shaba katika dutu kutokana na rangi ya kibichi

Kemia kichambuzi ni tawi la sayansi ya kemia. Inachunguza dutu mbalimbali kwa shabaha ya kujua viwango na hali za kemikali ndani yao.

  • uchambuzi stahilifu unachungulia ni kampaundi na elementi gani zilizopo katika dutu; unauliza je dutu hii ni nini? Kuna nini ndani yake?
  • uchambuzi wa kiasi unachungulia hizi kampaundi na elementi zinapatikana kwa kiasi gani
  • uchambuzi wa muundo unachungulia je molekuli za dutu zimepangwa namna gani, kwa mfano kwa fuwele au namna nyingine