Kampuni ya Viatu ya Hanover
Kampuni ya Viatu ya Hanover | |
---|---|
Jina la kampuni | Kampuni ya Viatu ya Hanover |
Ilianzishwa | 26 Desemba 1899 |
Mwanzilishi | Harper Donelson Sheppard C.N. Myers |
Huduma zinazowasilishwa | Utengenezaji |
Mmiliki | C & J Clark |
Makao Makuu ya kampuni | Hanover, Pennsylvania Ikahamishwa Virginia Magharibi katika mwaka wa 1996 |
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii | Viatu |
Nchi | Marekani |
Tovuti | Hanover Shoe Company |
Kampuni ya Viatu ya Hanover imo katika Hanover, Pennsylvania ilikuwa mojawapo ya kampuni kubwa za kuunda viatu na zenye mafanikio katika kata la York. Kuhusu jengo la kampuni hii:
- Pahali ilipokuwa: Hanover, Pennsylvania
- Mwaka uliojengwa: mwaka wa 1910
- Aina ya Jengo: Viwanda
- Mfumo wa Ujenzi: matofali, mawe, na kuni.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Bw. Harper Donelson Sheppard alizaliwa katika kata la Pitt ,eneo la Carolina Kaskazini mnamo tarehe 9 Oktoba 1868, akiwa mwana wa 13 katika familia ya watoto 15. Bw. Sheppard aliingia ushirikiano wa kibiashara na Bw. C.N. Myers na wakaanzisha kampuni ya Hanover mnamo 26 Desemba 1989 wakiwa na maono sawa.Maono yao yalikuwa kuuza viatu bora kabisa kwa bei moja , $ 2.50 kwa kila jozi, na kutokuwa na muuzaji wa rejareja kwa kuuzia umma wenyewe. Walifungua duka lao la kwanza huko York mnamo Juni 1900. Katika miaka mitano ya Kampuni ya Viatu ya Hanover,ilikuwa imeweza kufungua maduka 61 kutoka Indianapolis hadi Jiji la New York.[1]
Watu hao wawili (Myers na Sheppard) walichukua jukumu la kuendesha mipango ya kuendeleza jamii kama ujenzi wa hospitali ya Hanover General Hospital, uchapishaji wa gazeti la Evening Sun,kuchimbua mabwawa mawili,kuwasilisha huduma za maji kwa umma, kuunda uwanja wa michezo wa mtaa na kuanzisha Hanover Shoe Farms.[2]
Katika mwaka wa 1966, Kampuni ya Viatu ya Hanover ilifungua kiwanda cha utengenezaji huko Franklin,WV.Walichukua mikataba ya kuunda viatu kutoka kampuni za Bostonian na JC Penney na kuunda viatu hivyo chini ya jina la Hanover. Katika mwaka wa 1978, C & J Clark ilinunua Kampuni ya Viatu ya Hanover na ikahamisha makao yao makuu ya Amerika Kaskazini kutoka Hanover,PA.Operesheni za kampuni hii zilihamishwa hadi Virginia Magharibi katika mwaka wa 1996 kwa sababu ya kodi za nafuu katika eneo hilo. Jengo la hapo awali la Hanover Shoe lilikuwa katika barabara ya Carlisle Street huko Hanover,PA.Baada ya kukaa tupu bila kutumika tangu miaka ya 1970,lilibadilishwa kuwa jumba la makazi katika mwaka wa 2001. Jengo lao la kuzalisha kawi lilibadilishwa kuwa jumba la kumbukumbu la Idara ya Moto ya Hanover[3].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ^ - http://www.selectregistry.com/inns/qv/iid/340/cpid/382/custompage/bedandbreakfast.aspx Ilihifadhiwa 31 Januari 2009 kwenye Wayback Machine.
- ^ - http://www.selectregistry.com/inns/qv/iid/340/cpid/382/custompage/bedandbreakfast.aspx Ilihifadhiwa 31 Januari 2009 kwenye Wayback Machine.
- ^ - http://hsc.thomas-industriesinc.com/HSC_History.htm
Viungo Vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Hanover Shoe Company - Historia, sasa na yote yaliyopita.
- Historia