Kampuni ya HL Green

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kampuni ya H.L. Green

Kampuni ya H.L. Green ulikuwa mnyororo wa maduka madogo nchini Marekani katika karne ya ishirini ulioitwa jina hili kumkumbuka mwanzilishi Harold L. Green (1892-1951).

Mnyororo ulianzishwa katika mwaka wa 1932. Kampuni hiii iliendesha maduka 133 ya rejareja tangu mwaka wa 1935,mengi yakiwa yamenunuliwa kutoka mnyororo wa maduka ya Metropolitan Chain Stores(kampuni ambayo Harold Green alikuwa rais), F&W Grand Stores, Kampuni ya Isaac Silver na Ndugu zake na Kampuni ya F&W Grand-Silver Stores.

Harold David Kittinger, ambaye alikuwa mwanzilishi wa mnyororo wa Kittinger's uliokuwa umeungana na McLellan's, alikuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo tangu mwaka wa 1932 hadi alipoaga dunia katika mwaka wa 1947.Alipokuwa rais wa kampuni hii, mnyororo huu ulikuwa umekua hadi maduka 200. Ilimiliki pia maduka ya Shulte-United.

Ilipofika mwaka wa 1957,kampuni hii ilikuwa na maduka 227, na ilikuwa imeanza kuingia katika vituo vya ununuzi. Green ilinunua kampuni ya Olen, kapuni ya uuzaji bidhaa katika Mobile, Alabama. Maurice Olen akawa rais wa kampuni iliyoundwa kutokana na muungano huo lakini akatoka huko baada ya upelelezi kufichua kuwa kuna ukosfeu wa mali fulani.Hii ilisababisha uchunguzi kwa kampuni na Tume ya Marekani ya Usalama na Biashara na 'pia' kampuni ikafungua kesi na Olen. Olen alihukumiwa kwa mashtaka yale na kutozwa fainiya $ 2,500.

Ilinunua United Stores,iliyokuwa na sehemu kubwa ya umiliki katika kampuni za McCrory Stores na McLellan Stores lakini iliuzia Shirika la BTL katika mwaka wa 1960. Mwaka wa 1961,McCrory Stores ilijiunga na H.L. Green,kampuni ya muungano ikichukua jina la McCrory. Wiki iyo hiyo,ilitangazwa kuwa McCrory ilinunua Lerner Stores. H.L. Green iliuza maduka za ke zilizokuwa Kanada,Metropolitan Stores na mali zingine mbalimbali.Kufanya hivi kulipunguza maduka yaliyo katika mfumo wake kutoka 366 hadi 147.

Maduka yaliitwa H.L. Green baada ya McCrory kupata shida za kihela katika mwisho wa miaka ya 1990.

Ubaguzi[hariri | hariri chanzo]

Kama maduka mengi siku hizo, maduka yao ya Kusini mwa Marekani yalibagua kaunta zao hadi maandamano ya mwanzo wa miaka ya 1960 yalilazimisha yaache ubaguzi huo. Katika eneo la Kaskazini,meneja wa maduka kadhaa walichukua jukumu la kuacha ubaguzi katika kuajiri watu, hii ilifanyika katika mwanzo wa miaka ya 1950 huko Newark, New Jersey.

Hatimiliki[hariri | hariri chanzo]

Kampuni hii ilikuwa katika kesi kubwa dhidi ya Shapiro Bernstein ambapo muuzaji mmoja wa maduka ya HL Green aliuza rekodi za nyimbo zisizo halali.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]