Nenda kwa yaliyomo

Kampuni ya Green Flag

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya Kampuni ya Green Flag
Jina: Kampuni ya Green Flag
Nchi: Uingereza
Mwaka wa uanzilishi: 1971
Huduma: Urekebishaji wa shida za magari,Umekanika
Tovuti rasmi: http://www.greenflag.com

Green Flag ni kampuni ya kutoa usaidizi wa shida za magari barabarani iliyo na makao yake Uingereza.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Iliundwa katika mwaka wa 1971 ikiwa chama cha National Breakdown Recovery Club na ikaendeshwa chini ya jina hili ikimilikiwa na National Car Parks mpaka mwaka wa 1994,ndipo ikapewa jina jipya la Green Flag(Bendera ya Kijani Kibichi) kama jina lenye maana.

Baada ya ununuzi wa NCP na Cinven,kampuni hii ilinunuliwa na Direct Line katika mwaka wa 1999. Kufuatia ununuzi wa Direct Line na benki ya Royal Bank ya Scotland, Green Flag ni mojawapo wa kampuni za Kundi la RBS. Kwa miaka minne mfululizo,Green Flag imekuwa mshindi wa tuzo ya Your Money award for Best Direct Breakdown provider ya kampuni bora ya kuleta usaidizi katika shida za barabarani.

Tofauti kati ya kampuni hii na zingine

[hariri | hariri chanzo]

Ikiwa tofauti na kampuni za AA na RAC,Green Flag haina magari yake ya kazi au mekanika wake. Badala yake, kampuni hii ina mtandao wa mekanika katika mitaa mbalimbali. Mmojawapo ya faida za njia hii (kulingana na kampuni) ni kwamba kampuni za mitaa zina maarifa kuhusu eneo lao na hii inawawezesha kujibu wito za shida haraka zaidi. Kwa kutumia mfumo huu,kuna faida ya magari kama 86% kurekebishwa shida zao kando ya barabara. Green Flag ina wanachama milioni tano.

Mapema katika mwaka wa 2008,Green Flag ilipunguza ukubwa wa mtandao wao kwa karibu kampuni mia. Green Flag ilipeana zabuni ya kazi yake kwa watoaji huduma wakitilia maanani vitu kadhaa. Vitu hivi ni kama bei,eneo linalotaka kuhudumia ,ukubwa wa biashara na idadi ya maeneo ya kuhudumia. Makandarasi hawa wanaingia katika mnada dhidi ya kila mwingine ili kufika "lengo bei" lililowekwa. Green Flag imesema mfumo wake huu umefanikiwa sana; hata hivyo wakiwa na makampuni chini ya 100 ikifanya kazi nao madai yao ya kutumia maarifa ya mitaa kusaidia wanachama yamepoteza uhalali.

Muda wa wastani wa kuitikia wito wa Green Flag ni dakika 28,huandikwa dakika 30 katika tovuti yao rasmi na matoleo ya makala,hii inawapa nafasi ya kwanza katika orodha ya muda wa mwitikio wa kampuni za aina hiyo. Hii ilikadiriwa kwa wito 318,000 zilizokuwa kati ya mwezi wa 8 Agosti na 9 Machi.

Tovuti ya Green Flag pia ina ramani ya ambayo imepigiwa kura kama ramani bora kabisa kati kampuni tatu kubwa katika sekta hiyo ya huduma za barabarani.

Angalia Pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. a b Green Flag press pack March 2007 Ilihifadhiwa 8 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
  2. Your Money awards 2007

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]