Kampuni ya Bacup

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kampuni ya Viatu ya Bacup
Jina la kampuni Kampuni ya Viatu ya Bacup
Ilianzishwa 1928
Mwanzilishi Ernst Goodwin
Huduma zinazowasilishwa Utengenezaji
Makao Makuu ya kampuni Lancashire,Uingereza
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii Viatu
Nchi Uingeeza
Tovuti Tovuti rasmi ya Kampuni ya Bacup

Muhtasari[hariri | hariri chanzo]

Kampuni ya Viatu ya Bacup ni kampuni ya kutengeneza viatu iliyo na makao yake katika kijiji cha Stacksteads,karibu na Bacup, Lancashire,Uingereza. Kampuni hii ilianzishwa katika mwaka wa 1928 na Ernst Goodwin. Kampuni ya Bacup ni mojawapo ya kampuni bora, zinazojulikana kwa kuunda viatu, zilizofunga viwanda vyake katika mwisho wa miaka ya 1990 na kuanza kuagiza viatu kutoka Mashariki ya Mbali. Wanaowasilisha viatu hivyo wana makao yao nchini Uchina(nchi ambayo kampuni hii imeanzisha makao yake mpya),Vietnam na Uhispania.[1]

Ukuaji wa Kampuni ya Viatu ya Bacup[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka wa 1928, kampuni hii imenawiri na ikawa wasambazaji wengi, wa viatu vyao, katika nchi ya Uingereza.Makao yao makuu yalipatikana Stacksteads.

Sekta kuu za kampuni hii ni viatu vya Wanaume, Wanawake, Watoto na vya kutumika katika mazoezi ya michezo. Wameajiri wauzaji wa rejareja wanaojulikana sana kwa mfano Tesco,ASDA ,Woolworths na Littlewoods wakiwa wateja wao wakuu.

Katika mwaka wa 2002,kampuni hii ilifungua sehemu mpya iliyoitwa Alpha Logistics & Warehousing ya kuhusisha matumizi kamili ya maghala yao yote na matumizi bora ya wafanyikazi wenye vipaji.

Pamoja na upanuzi wa makao makuu ya kampuni hii,Bacup wameanzisha aina mpya ya viatu vya wasichana.Aina hii inaitwa Redfoot After Party Shoe na ni bidhaa za kampuni hii zilizosajiliwa katika sheria.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ Wide Fitting Famous Footwear and Famous Foot Care Products by - Natureform.co.uk
  2. ^ Lancashire County Council: Lancashire Profile
  3. ^ Retailing - UK News 1998
  4. ^ SHOEINFONET Wanted - Employee
  5. ^ Bacup Shoes

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]