Nenda kwa yaliyomo

Justus Nyang'aya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Justus Abonyo Nyang'aya ni mtaalamu wa maendeleo ya jamii na mwanaharakati wa haki za binadamu [1]ambaye alihudumu kama Kamishna katika Shirika la Uchaguzi la Kenya IEBC hadi 2 Desemba 2022.[2][3]Aliongoza kamati ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Yeye ni mmoja wa makamishna wanne kando na Juliana Cherera, Irene Masit, na Francis Wanderi ambao walikataa[4]matokeo ya urais katika uchaguzi mkuu wa Kenya wa 2022 [5][6][7] yaliyosomwa na Mwenyekiti Wafula Chebukati.

Kazi

Justus Nyang`aya alikuwa Mtaalamu wa Elimu ya Amani na UNESCO-PEER kwa mwaka mmoja hadi mwaka 1988 kabla ya kufanya kazi kama Mshauri wa Elimu ya Wakimbizi katika Windle Charitable Trust kwa miezi 27 kuanzia Machi 1988.

Alikuwa afisa mkuu mtendaji wa Inter Sudanese Consultations on Peace & Justice (ISCOP) kwa mwaka mmoja kuanzia mwaka 2004. Kuanzia katikati ya mwaka 2009 alihudumu kama Mkurugenzi wa Nchi [8]wa Amnesty International kwa zaidi ya miaka minane na nusu kabla. kuhamia hadi kuwa afisa mkuu mtendaji katika Leadership Education For Africa Development (LEAD Africa) mnamo Januari 2018 ambapo alifanya kazi kwa chini ya miaka minne kabla ya kuteuliwa kuwa kamishna katika IEBC mnamo 2 Septemba 2021 kwa muda wote.[9]Alijiuzulu tarehe 2 Desemba 2022.[10]

Elimu

Justus alipata elimu yake ya upili katika Shule ya Kanunga iliyoko Kiambaa, Kata ya Kiambu. Ana Stashahada ya Uongozi, Utawala, Amani na Mabadiliko ya Migogoro na Uongozi wa Shirika kutoka Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa, (Jordan) pamoja na Shahada ya Uzamili ya Sanaa (Elimu) kutoka Taasisi ya Elimu, Chuo Kikuu cha London.

Marejeo

  1. "Business Daily". Business Daily (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-06-08.
  2. Betty Njeru. "IEBC commissioner Justus Nyang'aya resigns amid probe". The Standard (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-06-08.
  3. "IEBC Commissioner Justus Nyang'aya resigns". The Star (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-06-08.
  4. "Cheo – Matokeo ya Kazi Nzuri", Peter DM Bwimbo: Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere, Mkuki na Nyota Publishers, ku. 105–114, 2015-11-03, iliwekwa mnamo 2024-06-08
  5. Ezra Nyakundi (2022-08-17). "Little Known Details of IEBC Commissioner Justus Nyang'aya Who Disputed Chebukati's Presidential Results". KDRTV (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-06-08.
  6. https://www.whispersnorth.com/justus-nyangaya-caught-at-the-centre-of-iebc-storm/
  7. "Nation - Breaking News, Kenya, Africa, Politics, Business, Sports | HOME". Nation (kwa Kiingereza). 2024-06-08. Iliwekwa mnamo 2024-06-08.
  8. Cyrus Ombati. "Amnesty International Kenya director shot, wounded in Ongata Rongai". The Standard (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-06-08.
  9. "Four new IEBC commissioners take oath of office". Citizen Digital (kwa Kiingereza). 2021-09-02. Iliwekwa mnamo 2024-06-08.
  10. "Nation - Breaking News, Kenya, Africa, Politics, Business, Sports | HOME". Nation (kwa Kiingereza). 2024-06-08. Iliwekwa mnamo 2024-06-08.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Justus Nyang'aya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.