Junior Madozein

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Joseph Junior Ghislain Madozein (alizaliwa tarehe 10 Oktoba 1987) ni mchezaji wa mpira wa kikapu na raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mara ya mwisho alichezea ASOPT inayoshiriki Ligi ya Kikapu Daraja la I nchini humo.[1]

Wasifu kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Madozei alichezea timu ya taifa ya mpira wa kikapu akiwakilisha nchi yao katika mashindano ya AfroBasket mwaka 2007, ambapo alipata wastani wa pointi 1.7, rebaundi 1.3, na pasi za magori 0.8. Mnamo Juni 26, 2015, alikuwa mmoja wa wachezaji 20 walioitwa kwenye kikosi cha timu hiyo kwahajili ya mashindano ya AfroBasket 2015 na kocha mkuu Aubin-Thierry Goporo. Wengine ni pamoja na Romain Sato na James Mays.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]