Nenda kwa yaliyomo

Juan de Salazar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu la JuanDeSalazar
Sanamu la JuanDeSalazar

Juan de Salazar y Espinoza alikuwa conquistador yaani mpelelezi na mwanajeshi Mhispania aliyeunda mji wa Asuncion katika Paraguay.

Alizaliwa 1508 katika Espinosa de los Monteros kwenye mkoa wa Burgos (Hispania). Akajiunga na kikosi cha Wahispania kilichosafiri kwenye mto Rio de la Plata mwaka 1535.

Akaongoza kikundi kilichofuata mto Paraguay na tarehe 15 Agosti 1537 alianzisha kituo cha kijeshi kilichoitwa "Nuestra Señora Santa María de la Asunción".

Baada ya kushiriki 1540 katika uasi dhidi ya gavana wa Río de la Plata Álvar Núñez Cabeza de Vaca alifukuzwa Amerika na kurudishwa Hispania. Akarudi mwaka 1547 na kati ya 1550 na 1555 akaongoza tena upelelezi wa Paraguay.

Akaaga dunia mjini Asuncion mwaka 1560.