Nenda kwa yaliyomo

Josco boy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Josco Boy
Jina la kuzaliwa Jonathan Aoso
Pia anajulikana kama Josco boy
Amezaliwa 28 Mei 2009 (2009-05-28) (umri 15)
Asili yake Mtanzania
Kazi yake Mwanamuziki
Aina ya sauti vocal
Miaka ya kazi 2020- Present

Jonathan Aoso (maarufu kwa jina lake la kisanii Josco boy; alizaliwa katika Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu[1], 28 Mei 2009) ni msanii wa kurekodi wa bongo Flava kutoka Tanzania.

Alianza kazi yake ya muziki mnamo mwaka 2020 akiwa na umri wa miaka 11 huku akiuza Miwa.[2]

Mwaka 2022 alitoa albamu yake ya kwanza iitwayo A Boy from Africa, ikifuatiwa na EP yake ya pili, Dunia, iliyotolewa Septemba 21, 2023. Mbali na kuwa mwimbaji, Josco Boy pia ni mtayarishaji wa muziki na mbunifu wa michoro. Anamiliki lebo yake ya muziki iitwayo ℗ Josco Boy Music Worldwide.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Nyimbo na Albamu Zinazovuma

[hariri | hariri chanzo]
  • 2022: Napendwa
  • 2022: Moyo Unauma
  • 2022: A Boy from Africa

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Josco Boy ana ndugu watano; kaka watatu na dada wawili. Mmoja wa dada zake, Msenwa, anaishi naye na mara kwa mara huonekana kwenye video zake za muziki na ana kituo chake cha YouTube.

Kwa sasa, Josco Boy anaendelea kukuza kipaji chake katika tasnia ya muziki nchini Tanzania na kimataifa.

  1. "Josco Boy". FilmFreeway (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-09.
  2. "Josco Boy's profile - Pianity". pianity.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-09.