Nenda kwa yaliyomo

K-Ci na Jojo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Jojo Hailey)
K-Ci na Jojo
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii K-Ci na Jojo
Nchi Marekani
Aina ya muziki R&B na Soul
Kazi yake Waimbaji
Miaka ya kazi mn. 1990 -
Ameshirikiana na Jodeci, Tupac
Ala Sauti
Kampuni Uptown/MCA

K-Ci na Jojo ni kundi la muziki wa R&B kutoka nchini Marekani, wakiwa ndugu kati ya Cedric Hailey (K-Ci Hailey aliz. 1969) na Joel Hailey (Jojo Hailey aliz. 1971). Wote wawili ni wazaliwa wa Charlotte, North Carolina, Marekani.
Pia walikuwa wanachama wa kundi la zamani la muziki wa R&B na Soul "Jodeci" na Ndugu wengine wawili ambao ni Donald Degrate (Devante Swing) na Dalvin Degrate (Mr. Dalvin) kwa pamoja wanaunda kundi la Jodeci.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wakiwa bado wadogo K-Ci na Jojo walikuwa waimbaji wa kwaya katika kanisa la Pentekoste, wakawa wanafanya matamasha mbali huku na kule.

Wakiwa katika baadhi ya matamasha wakutana na Devante Swing pamoja na kaka yake Mr. Dalvin Degrate, wakakaa pamoja na kujadilia kuunda kundi la muziki ambalo ndio linaloitwa Jodeci.

Akiwa ana miaka 16 Devante Swing alisafiri kwenda Minneapolis. Alipofika huko hakuwa mbali sana na masuala ya kimuziki hivyo akaamua kujiunga na Prince Organization, moja kati ya wanamuziki wa pop wa Marekani. Pamoja na kujiunga Prince Organization, Devante Swing hakufaulu kimuziki kama alivyokuwa anategemea.

Baadae akamtaka K-Ci na Jojo kujiunga nae huko New York katika duka fulani alilokuwa anafanya kazi ya kuuza kanda, ambalo zilikuwemo pia moja kati ya kazi alizofanya za muziki.

Siku moja wakiwa wanauza kanda za redio alipita msanii mmoja mkubwa (Heavy D) akazitia mkononi zile kanda na kuzipitisha katika Studio ya Uptown Records chini ya mmiliki wa Studio hiyo bwana Andre Harrell, ambaye ndiye aliyefanya maandalizi ya kuingia nao makataba wa kurekodi albamu, ndio hapo walipoanza muziki rasmi na kujiita Jodeci.

Wao kama Wao

[hariri | hariri chanzo]

Albamu Walizotoa

[hariri | hariri chanzo]
  • 1997: Love Always (Imesh. Naf. #6 Katika US Billboard 200)
  • 1999: It's Real (Imesh. Naf. #8 Katika US Billboard 200)
  • 2000: X (Imesh. Naf. #20 Katika US Billboard 200)
  • 2002: Emotional (Imesh. Naf. #61 Katika US Billboard 200)
  • 2005: All My Life: Their Greatest Hits (Imesh. Naf. #52 Katika US Billboard 200)
  • 2007: 20th Century Masters Nyimbo Mchanganyiko za K-Ci na JoJo

Nyimbo Maarufu

[hariri | hariri chanzo]
  • 1996: "How Could You"
  • 1997: "You Bring Me Up"
  • 1997: "Last Night's Letter"
  • 1998: "All My Life"
  • 1998: "Don't Rush (Take Love Slowly)"
  • 1999: "Tell Me It's Real"
  • 1999: "Girl"
  • 2000: "Life"
  • 2000: "Fee Fie Foe Fum"
  • 2001: "Crazy"
  • 2001: "Wanna Do You Right"
  • 2002: "This Very Moment"
  • 2003: "It's Me"

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu K-Ci na Jojo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.