Jimmy Needham

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Jimmy Needham
Jimmy Needham akiimba alipokuwa anapotoa kwa mara ya kwanza albamu yake ya Not Without Love akiwa Nashville, TN mnamo 24 Agosti 2008.
Jimmy Needham akiimba alipokuwa anapotoa kwa mara ya kwanza albamu yake ya Not Without Love akiwa Nashville, TN mnamo 24 Agosti 2008.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Jimmy Needham
Aina ya muziki Kikristo, Nyimbo za Kikristo za Kisasa
Kazi yake Mwanamuziki
Studio Inpop
Tovuti Tovuti Kamili ya Jimmy Needham

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jimmy Needham (amezaliwa 22 Agosti, 1985) ni mwanamuziki wa kisasa wa Kikristo wa Marekani aliye na mkataba na Inpop Records. Albamu yake ya pili na Inpop , Not Without Love, ilitolewa tarehe 19 Agosti 2008. Mapema katika mwaka wa 2008, alikuwa mgeni kwenye ziara ya mwimbaji wa Kikristo Natalie Grant.Ziara hii ilibandikwa jina la Relentless likimaanisha bila kuchoka.Jimmy alikuwa amezuru pamoja na Newsong,Echoing Angels na Nate Sallie mwishoni mwa mwaka wa 2007.

Yeye alifuzu kutoka Chuo Kikuu cha Texas A & M aliposomea historia na falsafa.

Vishawishi[hariri | hariri chanzo]

Katika albamu yake ya kwanza,Speak(Ongea katika lugha ya Swahili),Needham alieleza kuwa wanamuziki anaofuata mifano yao ni Jonny Lang, Lauryn Hill,Gavin DeGraw,Marc Broussard,Jason Mraz na hasa Keith Green. Needham alisema "Wakati mimi humsikiliza nahisi vizuri sana kwa kuwa mimi huhisi kuwa Mung ametupa roho sawa katika kile tunachotaka kuimba juu juu yake. Kama muziki - hasa muziki ya Kikristo - hainisababishi kutubu ama kumsifu Mungu basi sijui mbona niendelee kuisikiza. Na nadhani hii ndiyo sababu mimi nampenda Green Keith sana. Anazungumza juu ya vitu vizuri na afichi ukweli."

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Katika kazi ya ya muziki,Jimmy Needham ametoa albamu zifuatazo

Albamu[hariri | hariri chanzo]

Nyimbo Zake[hariri | hariri chanzo]

 • "Dearly Loved" (ilikuwa nambari 11 katika chati ya Top Contemporary Hit Songs, 4/27/07)
 • "Lost at Sea"
 • "Fence Riders" (nambari 14 ranked katika gazeti ya R&R 15 Desemba 2007)
 • "A Breath or Two"
 • "Huriccane"
 • "Firefly"
 • "Forgiven & Loved"

Nyimbo na albamu alizoshirikishwa[hariri | hariri chanzo]

 • 2007: iPop 2008, "Lost At Sea" (Inpop)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. "Diskografia ya Jimmy Needham". http://www.jesusfreakhideout.com/artists/JimmyNeedham.asp. 2008-04-09.
 2. "Natalie Grant aleta Ziara ya Relentless kwa wasikilizaji nchi nzima". http://www.ccmmagazine.com/news/headlines/11569839/. 2008-04-09.
 3. "Biografia ya Jimmy Needham". http://www.cmcentral.com/artists/1184.html. 2008-04-09.
 4. Inpop Records. "Jimmy Needham". http://www.christianitytoday.com/music/artists/jimmyneedham.html. 2008-12-28.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]