Nenda kwa yaliyomo

Jimbo la Kiroma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Jimbo la Kirumi)
Ramani ya Dola la Roma yaonyesha majimbo mnamo mwaka 120

Jimbo la Kiroma (Kilatini: provincia) lilikuwa kitengo kikubwa cha utawala cha Dola la Roma nje ya Italia.

Majimbo ya kwanza yalikuwa visiwa vya Sisilia na Sardinia. Roma ilimtuma afisa mwenye cheo cha praetor pamoja na kikosi cha wanajeshi kwa ulinzi wa maeneo haya mapya.

Majimbo yalitawaliwa na wanasiasa Waroma waliowahi kuwa na cheo cha juu kama vile konsul au praetor. Kwa kawaida magavana hawa walipewa nafasi hii kwa muda wa mwaka moja tu. Hii ilikuwa pia tatizo la uatawala wa Kiroma wakati wa jamhuri kwa sababu maafisa wale walijaribu mara nyingi kujitajirisha katika muda wa mwaka mmoja. Palikuwa na usemi "Maskini alifika kwenye jimbo tajiri, na tajiri aliondoka katika jimbo maskini."

Wakati wa Makaisari utaratibu ulibadilishwa. Kaisari aliangalia utawala pia akajitahidi kuzuia unyonyaji mkali. Augustus alitofautisha majimbo ya senati ambako magavana waliteuliwa na Senati na majimbo ya Kaisari alikomteua gavana mwenyewe.

Wakati wa Diokletiano majimbo yalipangwa katika dayosisi 12.