Nenda kwa yaliyomo

Jennifer Doudna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jennifer Anne Doudna (amezaliwa Februari 19, 1964) [1] ni mkemia wa Marekani ambaye amefanya kazi za mwanzo katika kugundua teknolojia ya uhariri jeni kwa kutumia Njia ya ''CRISPR'' pamoja na michango mingine ya muhimu kwenye tasnia za biokemia na jenetiki.

Doudna ni mmoja wa wanawake wa kwanza kupokea tuzo ya Nobel katika sayansi. Alipokea Tuzo ya Nobel katika Kemia mwaka 2020 pamoja na Emmanuelle Charpentier "kwa ajili ya kutafiti mbinu ya uhariri wa jenomu." [2]

Doudna ni professa wa chansela ya Li Ka Shing katika idara ya kemia na idara ya biolojia ya molekuli na seli katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley. Pia amekuwa Mtafiti katika Taasisi ya Matibabu ya Howard Hughes tangu mwaka 1997. [3]

  1. "Jennifer Doudna – American biochemist". Encyclopædia Britannica Online. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Oktoba 7, 2020. Iliwekwa mnamo Novemba 13, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Press release: The Nobel Prize in Chemistry 2020". nobelprize.org. Nobel Foundation. Oktoba 7, 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Januari 15, 2021. Iliwekwa mnamo Oktoba 7, 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Curriculum Vitae (Jennifer A. Doudna)" (PDF). Lawrence Berkeley National Laboratory. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo Januari 15, 2017. Iliwekwa mnamo Oktoba 24, 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)