James Siang'a

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
James Siang'a
Timu ya Taifa ya Kandanda
Kenya
Teams managed
YearsTeam
1999–2000Kenya
2001–2003Simba SC
2002Tanzania
2003–2004Express FC
2004–2005Moro United
2007Mtibwa Sugar
2009–Gor Mahia
† Appearances (Goals).

James Aggrey Siang'a ni mchezaji kandanda wa kimataifa wa kitambo wa Kenya. Kwa sasa yeye ni meneja hodari wa kandanda, amekuwa mkufunzi katika mataifa mengi barani Afrika katika viwango vya vilabu na vya kitaifa, na hivi majuzi alikuwa mkufunzi wa klabu ya Gör Mahia.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Wasifu wake wa Uchezaji[hariri | hariri chanzo]

Siang'a alicheza kama mlinda lango na alicheza katika kiwango cha kimataifa kwa timu ya kitaifa ya Kenya.

Wasifu wa Ukocha[hariri | hariri chanzo]

Siang'a alikuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Kenya kati ya miaka ya 1999 na 2000, kisha akahamia nchi ya Tanzania, ambapo alikuwa meneja wa timu ya kandanda ya taifa mwaka wa 2002.[1]

Siang'a pia alikuwa mkufunzi wa klabu za Tanzania za Simba SC na Moro United na vilevile Express FC ya Uganda.

Mnamo Oktoba mwaka wa 2004, akiwa bado katika klabu ya Moro United, Siang'a aliombawa kuchukua nyadhifa ya kuwa meneja wa timu ya taifa ya Kenya lakini alikataa.[2] Baadaye mwezi huo, Siang'a pia aliombwa kuchukua nyadhifa ya umeneja kwa timu ya kitaifa ya Tanzania na kwa mara nyingine tena, alikataa.[3] Siang'a pia alikuwa mkufunzi wa timu ya Mtibwa Sugar nchini Tanzania, kabla ya kuwa kocha wa Gör Mahia nchini Kenya.[4][5]

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Emmanuel Muga (20 Julai 2002). Taifa stars in crisis. BBC Sport. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2009.
  2. Emmanuel Muga (31 Machi 2004). Siang'a demands his share. BBC Sport. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2009.
  3. Emmanuel Muga (29 Oktoba 2004). Tanzania appoint Phiri. BBC Sport. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2009.
  4. Robin Toskin (7 Aprili 2009). Siang'a's future at Gor in doubt. The Standard. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2009.
  5. Sammy Kitula (12 Aprili 2009). Gor coach Siang'a a man under siege. Daily Nation. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2009.
  6. Simba win Cecafa Club Cup. BBC Sport (4 Machi 2002). Iliwekwa mnamo 28 Mei 2009.
Flag of Kenya.svg Makala hii kuhusu Mchezaji Soka wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu James Siang'a kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.