James Abbott (mwanakandanda)
Mandhari
James Abbott (alizaliwa Patricroft, Uingereza, 1892; tarehe ya kufariki haijulikani) alikuwa mwanakandanda wa Manchester City iliyokuwa ikishiriki ligi kuu Uingereza.
Kabla ya vita ya kwanza ya Dunia, alicheza michezo mitatu akiwa na Manchester City akifunga magoli mawili kwenye michezo mitatu, likiwemo goli la mchezo dhidi ya Sheffield United mnamo mwezi wa 9 mwaka 1913. Alihamia klabu ya Hyde Road baada ya kutopata nafasi ya kucheza kwenye vilabu vya Barton Albion na Eccles Borough.