Jaha Dukureh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jaha Dukureh

Jaha Dukureh (alizaliwa kati ya mwaka 1989 au 1990) ni mwanamke mwenye asili ya Gambia, mwanaharakati wa haki za wanawake na mpingaji wa ukeketaji kwa wanawake[1].

Alikuwa mhanga wa ukeketaji wiki moja tu baada ya kuzaliwa. [2][3]. Ni mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa 'Safe Hands for Girls', taasisi inayofanya kazi ya kutokomeza ukeketaji, na ndiyo iliongoza katika 'The Guardians End FGM Global Media Campaign'.

Mwezi Aprili mwaka 2016 jina lake lilitajwa katika orodha ya 'Time 100'. Aliteuliwa kuwania tuzo ya Amani ya Nobel Februari 2018, ameshinda medali ya Eleanor Roosevelt Val-kill, na ubalozi wa kujitolea kwa Afrika.

Filamu kuhusu maisha yake ilikuwa itolewe na kampuni ya Accidental Picture na The Guardian.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Topping, Alexandra (12 May 2014). "Jaha Dukureh: 'In Washington, they don't want to talk abouvaginas'". The Guardian. Iliwekwa mnamo 11 June 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. http://www.safehandsforgirls.org/
  3. Daly, Claire (21 April 2016). "Time 100: FGM campaigner Jaha Dukureh makes prestigious list". The Guardian. Iliwekwa mnamo 11 June 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jaha Dukureh kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.