Jacobs University Bremen
Chuo Kikuu cha Jacobs Bremen (zamani Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Bremen, IUB) ni chuo kikuu cha binafsi mjini Bremen, Ujerumani.
Chuo Kikuu cha Jacobs ni taasisi inayotoa elimu ya juu iitumia Kiingereza kama lugha ya mafunzo tofauti na vyuo vya serikali. Chuo Kikuu cha Jacobs hulenga kuunganisha mifumo ya kitaaluma ya Kimarekani, Kiingereza na Kijerumani pamoja ili kutengeneza mazingira shirikishi baina ya michepuo mbalimbali na masomo tofauti.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Chuo Kikuu cha Jacobs kilianzishwa mnamo mwaka 1999 kama 'Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Bremen (IUB)' ila mnamo mwanzoni mwa mwaka 2007 kilibadili jina kama ishara ya utambuzi/shukrani ya ufadhili wa mhisani Klaus Johann Jacobs, aliyeinusuru IUB kufilisika.
Chuo hiki kilianzishwa kufuatia ushirikiano wa awali baina ya serikali ya jimbo la Bremen, Chuo Kikuu cha Bremen na Chuo Kikuu cha Rice cha Marekani.
Mwaka 2006 chuo hiki cha binafsi kilikuwa na matatizo ya kifedha na wakati ule taasisi ya Jacobs Foundation iliamua kutoa mchango wa € milioni 200 na kuchukua theluthi mbili za hisa ya shirika la chuo kikuu.
Kuanzia mwaka 2005 Chuo Kikuu cha Jacobs kimethibitishwa kama taasisi rafiki kwa familia na Hertie Foundation kufuatia uanzishwaji wa hatua maalum kwa wanachuo wenye majukumu ya kifamilia. [1]
Hivi karibuni Kituo cha Matangazo cha Deutsche Welle kilirusha matoleo 5 ya televisheni yaliyoitwa "Leaders of Tomorrow" (Viongozi wa Kesho) yaliyokilenga Chuo Kikuu cha Jacobs [2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-01. Iliwekwa mnamo 2010-11-10.
- ↑ [1]
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Official Website Archived 25 Mei 2021 at the Wayback Machine.
- Graduate Student Association at Jacobs University Archived 23 Juni 2011 at the Wayback Machine.
- Alfried Krupp College Archived 9 Septemba 2019 at the Wayback Machine.
- Mercator College Archived 3 Machi 2021 at the Wayback Machine.
- College III Archived 4 Novemba 2010 at the Wayback Machine.
- College Nordmetall