Ivan Gazidis
Ivan Gazidis (alizaliwa Johannesburg, Afrika Kusini, Septemba 13, 1964) ni mfanyabiashara na mchezaji wa zamani wa soka wa Afrika Kusini na Ugiriki ambaye alishika nafasi ya uongozi katika klabu ya A.C. Milan ya ligi kuu ya Italia Serie A.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Mwenye asili ya Kigiriki, Gazidis alizaliwa huko Afrika Kusini. Akiwa na umri wa miaka 4, alihamia Uingereza na baadaye alijiunga na shule ya kujitegemea ya Manchester Grammar na St Edmund Hall katika Chuo Kikuu cha Oxford, ambapo alipewa tuzo ya blue mara mbili kwa kucheza soka dhidi ya Cambridge mnamo 1984 na 1985.[1] Alishiriki katika masomo ya sheria na kuhitimu na shahada ya sheria mnamo 1986 na mwaka wa 1992 alihamia Marekani kufanya kazi kwa kampuni ya Latham & Watkins.[2]
Mwaka wa 1994, alijiunga na timu ya uanzishaji ya Major League Soccer, akawa naibu kamishna wa ligi hiyo mwaka 2001. Alisimamia maamuzi muhimu ya kimkakati na biashara ya MLS na kitengo chake cha masoko, Soccer United Marketing, ambapo alikuwa rais.[3] Pia alisaidia kuendeleza Shirikisho la Soka la Mexico (Mexican Football Federation) na Kombe la Dhahabu la CONCACAF.[3]
Mnamo Novemba 2008, Gazidis alikubali nafasi ya mkurugenzi mtendaji wa Arsenal, ambayo alianza rasmi tarehe 1 Januari 2009.[4] Aliyachukua majukumu ya mkurugenzi mtendaji wa zamani Keith Edelman na alitarajiwa kuchukua majukumu mengi yaliyofanywa awali na aliyekuwa makamu mwenyekiti David Dein.
Katika msimu wa 2017-18, alisimamia mabadiliko muhimu ya wafanyakazi katika klabu hiyo kwa maandalizi ya kuondoka kwa meneja wakati huo Arsene Wenger, ambaye tangazo lake lilitolewa mnamo Aprili 2018.[5] Gazidis aliongoza utafutaji wa Meneja mpya, hatimaye akimchagua Unai Emery mnamo Mei.
Baada ya kutangaza kuondoka kwake, ilifichuliwa kuwa watu wanaomfuata watakuwa Vinai Venkatesham kama Mkurugenzi Mtendaji, na Raul Sanllehi kama mkuu wa soka.[6]
Tarehe 18 Septemba 2018, Gazidis alitangaza kuwa ataondoka Arsenal kujiunga na A.C. Milan.[7] Alipokea jukumu hilo tarehe 1 Desemba 2018.[7] Katika dirisha la uhamisho la Januari 2020, aliamua kusitisha mkataba wa mkopo wa Gonzalo Higuain miezi sita kabla ya muda uliopangwa. Aliidhinisha uhamisho wa Krzysztof Piątek na Lucas Paquetá, ambao wote walitekelezwa na Leonardo.[8] Katika msimu wake wa kwanza kama Mkurugenzi Mtendaji wa klabu, timu ilimaliza ya tano katika Serie A, ambayo ilikuwa matokeo bora zaidi katika miaka sita. Na miaka miwili tu baadae, timu ilimaliza ya pili katika msimu wa Serie A 2020-2021; hii iliwawezesha kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wa UEFA kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2012-2013. Msimu uliofuata, A.C. Milan ilishinda Serie A kwa mara ya kwanza katika miaka 11.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Oxford University Association Football Club Varsity Alumni". OUAFC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-16. Iliwekwa mnamo 2023-06-10.
- ↑ "Ivan Gazidis named CEO of Arsenal", MLSNet.com, 26 November 2008. Retrieved on 2023-06-10. Archived from the original on 2009-07-13.
- ↑ 3.0 3.1 Wilson, Jeremy. "Arsenal end search for new chief executive with appointment of Ivan Gazidis", Daily Telegraph, 26 November 2008.
- ↑ "Arsenal name new chief executive", BBC Sport, 28 November 2008.
- ↑ "Arsenal Hires Outgoing Barcelona Director of Football Raul Sanllehi - The Page Magazine". 28 Novemba 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-15. Iliwekwa mnamo 2023-06-10.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Benge, James (18 Septemba 2018). "Gazidis leaves Arsenal to join AC Milan". www.standard.co.uk.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 7.0 7.1 "Ivan Gazidis: Arsenal chief executive leaves club to join AC Milan". 18 Septemba 2018 – kutoka www.bbc.co.uk.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "AC Milan News - Latest and real time updates". AC Milan.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ivan Gazidis kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |