Nenda kwa yaliyomo

Irene Sewankambo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Irene Kaggwa Sewankambo ni mhandisi wa umeme wa Uganda na mtendaji mkuu wa shirika, anahudumu kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) kuanzia tarehe 10 Februari 2020. [1]

usuli na Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Irene alizaliwa Uganda na alisoma Shule ya Msingi ya Kitante huko Kampala, Uganda. Alisoma Chuo cha Mount Saint Mary's Namagunga kwa elimu yake ya kati na ya upili. Alihitimu na stashahada ya Sekondari ya Hisabati, Fizikia na Kemia. Kisha akasoma Chuo Kikuu cha Makerere kusomea uhandisi wa umeme. [2]

Ana Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Uhandisi wa Umeme, aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, chuo kikuu kikongwe na kikubwa zaidi cha umma nchini Uganda. Shahada yake ya pili ya sayansi ya mawasiliano na mawimbi kutoka na Chuo Kikuu cha Bristol . Pia ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Usimamizi wa Uchumi na Sera kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde.[3]

Mara tu kabla ya uteuzi wake wa sasa, Mhandisi Sewankambo alihudumu Mkurugenzi wa Uhandisi na Miundombinu ya Mawasiliano katika Tume ya Mawasiliano ya Uganda. [4] Kabla ya hapo, alikuwa mkuu wa kitengo cha utafiti na maendeleo UCC na vile vile mratibu katika ofisi ya mkurugenzi mkuu. [5]

Mnamo Februari 2020, Judith Nabakooba, Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano alimteua Irene Sewankambo kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, akisubiri kuteuliwa kua mkurugenzi mtendaji mkuu. Alichukua nafasi ya Mhandisi Godfrey Mutabazi, ambaye kandarasi zake mbili mfululizo za miaka mitano zilikuwa zimeisha. [6]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Irene Kaggwa Sewankambo ni mwanamke aliyeolewa [6] na mwenye watoto. [7]

Angalia pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Christine Kasemiire (7 Februari 2020). "Why Minister Nabakooba appointed Irene Sewankambo to replace Mutabazi at UCC". Iliwekwa mnamo 8 Februari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Phionah Nassanga (27 Juni 2020). "I Didn't Get A Red Carpet Because I Am A Woman, Says UCC Boss". Iliwekwa mnamo 28 Juni 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. World Summit Awards (2018). "Irene Kaggwa Sewankambo: Head of Research & Coordinator, Office of the Executive Director, Uganda Communications Commission". World Summit Awards. Iliwekwa mnamo 8 Februari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Uganda Communications Commission (2019). "Irene Kaggwa Sewankambo: Director Engineering and Communications Infrastructure, Uganda Communications Commission". Uganda Communications Commission. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-03-08. Iliwekwa mnamo 8 Februari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. World Summit Awards (2018). "Irene Kaggwa Sewankambo: Head of Research & Coordinator, Office of the Executive Director, Uganda Communications Commission". World Summit Awards. Iliwekwa mnamo 8 Februari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)World Summit Awards (2018). "Irene Kaggwa Sewankambo: Head of Research & Coordinator, Office of the Executive Director, Uganda Communications Commission". Salzburg, Austria: World Summit Awards
  6. 6.0 6.1 Christine Kasemiire (7 Februari 2020). "Why Minister Nabakooba appointed Irene Sewankambo to replace Mutabazi at UCC". Iliwekwa mnamo 8 Februari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Christine Kasemiire (7 February 2020). "Why Minister Nabakooba appointed Irene Sewankambo to replace Mutabazi at UCC". Daily Monitor. Kampala
  7. Phionah Nassanga (27 Juni 2020). "I Didn't Get A Red Carpet Because I Am A Woman, Says UCC Boss". Iliwekwa mnamo 28 Juni 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Phionah Nassanga (27 June 2020). "I Didn't Get A Red Carpet Because I Am A Woman, Says UCC Boss". Daily Monitor. Kampala

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]