International School of Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

International School of Kenya ni shule ya kimataifa inayofunza wanafunzi kuanzia darasa la chekechea hadi darasa la 12. Shule hii iko nje ya jiji la Nairobi, Kenya. Ilianzishwa mwaka wa 1976 iliyojengwa katika uwanja wa hekta 25. Wanafunzi wanaweza kusomea mfumo wa elimu wa diploma ya Amerika ya Kaskazini au diploma ya International Baccalaureate. Shule hii inatambulika na MSA, na ni shule kubwa zaidi ya kimataifa mjini Nairobi. Shule hii pia ni mwanachama wa Chama cha Association of International Schools in Africa (AISA).

Mipangilio[hariri | hariri chanzo]

Shule hii ilianzishwa kutoka Nairobi International School (NIS) mnamo 1969, lakini matatizo ya kifedha iliilazimu Ubalozi wa Marekani na Ubalozi wa Kanada kuchukua uendeshaji wa shule hii mwaka wa 1976, na kuibadilisha jina kuwa Intrnational School of Kenya. ISK, kama inavyojulikana, imegawanywa katika shule tatu: ya Shule ya Msingi inayofundisha wanafunzi kutoka chekechea hadi darasa la 5, Shule ya Kati inayofundisha darasa 6-8, na Shule ya Upili inayofundisha darasa za 9-12.

Kila shule ina mwalimu wake mkuu na mshauri, na kwa kiasi kikubwa ina walimu wake, ingawa baadhi ya masomo hufundishwa na walimu sawiya. Walimu ni wengi hutoka Kanada, Marekani na Uingereza, na hata nchi nyinginezo.

Vifaa[hariri | hariri chanzo]

Kila shule ina madarasa yake na na vyumba vya burudani; hata hivyo shule zote tatu hutumia vifaa vingine kwa pamoja kama vile maktaba, mkahawa, na vifaa vya michezo na sanaa. Kituo chake cha Sanaa kilicho na thamani ya dola milioni nyingi inayosifika kuwa kituo bora zaidi mjini Nairobi. Shule hii ina chumba kikubwa cha kufanyia mazoezi, bwawa la kuogelea lenye maji ya moto, na viwanja tele vya kucheza. Mwaka wa 2006, mradi wa ujenzi ulianza ili ya kupanua shule ya sekondari. Ilmalizwa kujengwa mnamo Desemba 2007, na wanafunzi waligurishwa mwezi uliofwatia.

Shule hii pia inajulikana kwa michezo yake kama mpira wa kikapu, kriketi, mpira wa kandanda, voliboli, na kuogelea. Kila mwaka, wanafunzi wa shule ya sekondari hushiriki katika mashindano ya kimataifa ya ISSEA kwenye michezo ya mpira wa kikapu, kandanda, na voliboli.

Shule hii iko nje ya jiji la Nairobi mwishoni mwa barabara ya Peponi na imezungukwa na mashamba ya kahawa. Hata hivyo, ujenzi unaoendelea inaweza kubadili maeneo jirani.

Wanafunzi[hariri | hariri chanzo]

Chama cha wanafunzi ina zaidi ya wanafunzi 700 ikiwakilisha mataifa 74 tofauti. Zaidi ya robo ni Wamarekani, na wengineo wakitoka nchini Kenya, Uingereza, Kanada, Sweden na Uholanzi.

Mbegu maarufu ni kama: Dan Eldon (mpiga picha maarufu aliyeuwawa katika mgogoro wa Somalia mnamo 1993). Wahitimu wa shule hii wamewahi kujiunga na vyuo vikuu maarufu nchini Marekani (kama chuo kikuu cha Ivy League), Kanada, Uingereza, Australia, Afrika ya Kusini na Chama cha Umoja wa Ulaya.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]