Immature

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Immature
Taarifa za awali
Pia anajulikana kamaIMx
AmezaliwaLos Angeles, California, U.S.
Miaka ya kazi1990–2002, 2009–present
Studio
Ameshirikiana na
Wavutihttp://immatureofficial.com/
Wanachama
Marques Houston
Jerome Jones
Kelton Kessee
Don Santos
Marques Houston, mwimbaji mkuu wa bendi ya Immature/IMx

Immature (baadaye wakafahamika kama IMx) ni kundi la vijana la muziki wa R&B kutoka nchini Marekani. Kundi linasimamiwa na mtayarishaji wa rekodi Chris Stokes.

Wanachama wake ni pamoja na Marques "Batman" Houston (amezaliwa Agosti 4, 1981), Jerome "Romeo" Jones (amezaliwa Oktoba 25, 1981), na Kelton "LDB" Kessee (amezaliwa Januari 2, 1981), wote wakiwa wazawa wa Los Angeles, California, mahali ambapo ndipo kundi lilipoanzishwa.

Kundi limetoa albamu nne chini ya mwamvuri wa jina la Immature. Albamu hizo ni pamoja na: On Our Worst Behavior (1992; albamu pekee iliyohusisha mwanachama wa awali Don "Half Pint" Santos, baadaye nafasi yake ikachukuliwa na Kessee), Playtyme Is Over (1994), We Got It (1995) na The Journey (1997).

Ilipotimu mwaka wa 1999, kundi likabadili jina lao na kuwa IMx. Ilipotimu miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, wakatoa albamu mbili. Nazo ni Introducing IMx na IMx, vilevile wakatoa albamu yenye vibao mseto vilivyotamba yenye jina la Greatest Hits mnamo mwaka wa 2001.[1]

Kundi pia likajutupa katika uwanja wa tasnia ya maigizo. Wakashiriki katika filamu kama vile House Party 3 na House Party 4: Down to the Last Minute) na upande wa runinga walikuwemo kwenye A Different World, Sister, Sister, Family Matters, Soul Train na All That) kabla ya kila mtu kwenda safari yake mnamo mwaka wa 2002.

Mwaka wa 2010, Houston alitangaza kupitia kipindi cha runinga cha hip hop & R&B cha 106 & Park kwamba kundi linapanga kurekodi albamu nyingine itoke mwaka wa 2011. Baadaye wakatoa taarifa ya albamu kuwa jikoni kwa jina la "Forever Immature." Ilipangwa kutolewa katika majira ya joto ya mwaka wa 2013, ikiwa pamoja na ziara, walakini, tarehe ya kutolewa haikutolewa kwa mradi huo. Mnamo tarehe 6 Novembea, 2013, Immature walitumbuiza onyesho lao la kwanza tangu warudi tena mzigoni katika ukumbi wa Club Nokia jijini Los Angeles wakiwa na bendi nyingine Next na Dru Hill.

Mnamo mwezi wa Septemba 2019, Immature walitangaza ziara yao iliyopewa jina la #TBTour wakisindikizwa na Ray J, B5 a J. Holiday.[2]

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Immature ilianzishwa mjini Los Angeles, California mnamo mwaka wa 1990 na Marques "Batman" Houston, Jerome "Romeo" Jones na Don "Half-Pint" Santos. Kelton "LDB" Kessee (mpiga dramzi wa kundi) alijiunga mazima mnamo mwaka wa 1994, akichukua nafasi ya Santos ambaye wazazi wake walitaka aachane kabisa na masuala ya muziki. Hata hivyo walicheza pamoja katika filamu ya House Party 3. Mwaka wa 1999, kundi lilibadili jina lao kuwa IMx, wakidhani ya kwamba Immature haikisi tena maana ya bendi kwa vile washakuwa watu wazima.

Baada ya IMx[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka wa 2002, kundi likafa. Houston na Jones (chini ya jina la Young Rome) wakaanza kazi za kujitegemea, wakati huo Kessee aliendelea kuwa kama mtayarishaji wa rekodi. Houston akawa mwanachama wa kwanza wa zamani kutoa albamu ya kujitegemea iliyokwenda kwa jina la MH mnamo 2003.

Jones akafuata njia hiyohiyo kwa kutoa albamu ya kwanza mnamo mwaka wa 2004, yenye jina la Food for Thought. Houston baadaye akatoa albamu tano zaidi. Albamu hizo ni pamoja na: Naked (2005), Veteran (2007), Mr. Houston (2009), Mattress Music (2010) na Famous (2013).

Houston naJones pia wamewahi kufanya karia za uigizaji katika filamu za kucheza kama vile You Got Served (2004). Houston amecheza kama nyota mshiriki kwenye Fat Albert (2004) akaangukia katika uhusika mkuu kwenye ucheshi wa UPN Cuts. Mwaka wa 2007, alicheza katika filamu ya kutisha Somebody Help Me. Pia amepata kuonekana kama Roger kwenye onyesho la Sister, Sister (1994–1998).

Kazi ya muziki[hariri | hariri chanzo]

Immature[hariri | hariri chanzo]

On Our Worst Behavior[hariri | hariri chanzo]

Playtyme Is Over[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Playtyme Is Over

We Got It[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: We Got It (album)

The Journey[hariri | hariri chanzo]

Introducing IMx[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Introducing IMx

IMx[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: IMx (albamu)

Remember[hariri | hariri chanzo]

(2015 EP Albamu)

Kazi zingine[hariri | hariri chanzo]

Members[hariri | hariri chanzo]

Wanachama wa sasa[hariri | hariri chanzo]

Wanachama wa zamani[hariri | hariri chanzo]

  • Don "Half Pint" Santos – mwimbaji msaidizi, mghani (1990-1993)

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Diskografia ya IMx

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kigezo:IMx Kigezo:Marques Houston