Nenda kwa yaliyomo

Ida B. Wells

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wells C, 1893

Ida Bell Wells-Barnett ( Alizaliwa Julai 16, 1862 na Kufariki Machi 25, 1931) alikuwa mwandishi wa habari wa uchunguzi wa Marekani, alikua pia mwalimu na kiongozi wa harakati za kiraia. Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Kitaifa cha Maendeleo ya Watu wenye Rangi[1]. Wells alijitolea kwa kupambana na chuki, vurugu na kutetea usawa kwa watu waliokua na asili ya Afrika- Amerika pamoja na haki za wanawake[2].

Katikati ya miaka ya 1890, Wells aliandika makala ya lynching nchini Marekani na kupitia vipeperushi kama vile Southern Horrors: Law Lynch in all its Phases na The Red Record ambazo zilifichua uongo uliosikika kwa wazungu wakati huo watu weusi walikua na hatia ya uhalifu. Wells alifichua ukatili wa lynching na kuuchambua kwakutumia sosholojia yake, Alisema wazungu walikua wakitumia sheria ya lynching kuwakandamiza waafrika amerika waliokua wanaishi kusini mwa Marekani kwasababu waliawakilisha ushindani wa kiuchumi na kisiasa na hivyo kuwatishia wazungu kupoteza nguvu. Wells alilenga kuonyesha ukweli juu ya vurugu na kutoa maoni juu ya kuzuia vurugu hizo[3].


Wells alizaliwa katika utumwa huko Holly Springs, Mississippi. Akiwa na umri wa miaka 16, wazazi wake na kaka yake mdogo walifariki kwa kupata ugonjwa wa homa ya manjano mwaka 1878. Alianza kufanya kazi na kuwasaidia familia yake pamoja na bibi yake. Baadae alihama pamoja na ndugu na kwenda Memphis, Tennessee. Wells alipata mshahara mzuri alivoanza kazi ya uwalimu. Alishiriki kuandika ripoti kwenye gazeti la Memphis Free Speech na Headlight, ambapo ripoti hio iliangazia matukio ya ubaguzi wa rangi na ukosefu wa usawa.

Maisha Ya Mwanzo

[hariri | hariri chanzo]
Nyumba ya Bolling-Gatewood. Familia ya Wells iliishi katika vibanda vilivyopo nyuma ya nyumba hii wakati wakimilikiwa na Spires Bolling.

Ida Bell Wells alizaliwa katika shamba la Bolling karibu na Holly Springs, Mississippi[4]. Alizaliwa mnamo Julai 16, 1862. Ida Wells alikuwa ni mtoto wa kwanza wa James Madison Wells (1840-1878) na Elizabeth "Lizzie" (Warrenton). James Wells alikua mtumwa, mama yake aliyeitwa Peggy nae alikua mtumwa ambaye alizaa na mzungu aliyekua ni mmiliki wake. James akiwa na miaka 18, Baba yake alimpeleka James Holly Springs na kumwajiri kama fundi seremala kwa Spires Bolling na mshahara wake alipewa baba yake (Mmiliki wake). Mmoja kati ya watoto kumi waliozaliwa katika shamba lililopo Virginia, Lizzie alitekwa nyara na kusafirishwa kutoka kwa familia yake na ndugu zake, ambapo alijaribu kutafuta familia yake bila mafanikio na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe[5]. Lizzie alikua akimilikiwa na Spires Bolling, alikua anafanya kazi za nyumbani. Kabla ya tangazo la ukombozi kutolewa wazazi wake Wells walikuwa watumwa wa Bwana Spires Boiling na kuzaa watoto ilihali wakiwa katika utumwa. James Wells alijenga sehemu kubwa ya nyumba ya Bolling-Gatewood, ambayo Spires Bolling aliishi. Nyumba ya Bolling-Gatewood kwasasa imekuwa Nyumba ya Makumbusho ya Ida B. Wells-Barnett[6]. Familia ya Wells iliishi mahali pengine katika mali za Spires Bolling.


Baada ya ukombozi, Baba yake Wells alikua mdhamini wa Chuo cha Shaw (Sahivi Chuo cha Rust). Alikataa kuwapigia kura wagombea wa chama cha Democratic, alikua mwanachama wa Loyal League, alikua akijulikana kama "race man" kufuatia kujihusisha kwake katika siasa na kujitolea katika chama cha Republican[7]. Alifanikiwa kwa kuanzisha biashara ya useremala huko Holly Springs mnamo 1867 na mke wake alijulikana kama mpikaji maarufu "famous cook"[8].

  1. "Ida B. Wells", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-04-22, iliwekwa mnamo 2024-04-22
  2. "Ida B. Wells", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-04-22, iliwekwa mnamo 2024-04-22
  3. "Paula Giddings", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-02-06, iliwekwa mnamo 2024-04-22
  4. "Ida B. Wells", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-04-22, iliwekwa mnamo 2024-04-22
  5. "Ida B. Wells", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-04-22, iliwekwa mnamo 2024-04-22
  6. "Ida B. Wells", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-04-22, iliwekwa mnamo 2024-04-22
  7. "Ida B. Wells", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-04-22, iliwekwa mnamo 2024-04-22
  8. "Ida B. Wells", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-04-22, iliwekwa mnamo 2024-04-22