Nenda kwa yaliyomo

Hospitali ya Bulongwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hospitali ya Kilutheri ya Bulongwa inapatikana mkoa wa Njombe na inamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ya Kusini Kati.

Hospitali hii ilifunguliwa mwaka 1968. Hospitali ya kilutheri ya Bulongwa ni hospitali ya rufaa yenye vitanda 120. Inapata misaada kutoka serikalini kupitia wizara ya afya kwa ajili ya wafanyakazi 27 na vitanda 90 tu. Hospitali hii inahudumia watu wapatao 60,000. Kuna wodi tano katika hospitali hii ya Bulongwa ambazo ni wodi ya wazazi, wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, wodi ya watoto na wodi ya urekebishaji. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]