Hope & Faith
Mandhari
Hope & Faith | |
---|---|
Nembo ya Hope & Faith | |
Aina | Mchezo wa kuchekesha |
Imetungwa na | Joanna Johnson |
Nchi inayotoka | Marekani |
Lugha | Kiingereza |
Ina misimu | 3 |
Utayarishaji | |
Muda | makisio ni dk. 30 |
Urushaji wa matangazo | |
Kituo | ABC |
Inarushwa na | 26 Septemba 2003 |
Viungo vya nje |
Hope & Faith ni kipindi cha kuchekesha cha Marekani iliyoonyeshwa kuanzia 26 Septemba 2003 hadi 2 Mei 2006 kwa misimu mitatu kwenye stesheni ya ABC.
Kipindi hiki kilikuwa na waigizaji wakuu: Faith Ford na Kelly Ripa. Hope Shanowski (Ford) alikuwa na mume na watoto watatu. Faith Fairfield (Ripa) alikuwa muigizaji maarufu na nduguye Hope. Kipindi hiki inatokana na maisha ya mbunifu Joanna Johnson - ambaye alikuwa mhusika katika kipindi maarufu cha The Bold and the Beautiful. Kipindi hiki kilishirikisha wasanii wengine kama Tony Curtis, Dean Cain, Robert Wagner, Regis Philbin, Kathie Lee Gifford, Jenny McCarthy, Jaclyn Smith, Louise McCafferty na Mark Consuelos.
Kipindi hiki kilirekodiwa mjini New York City kwenye Silvercup Studios.
Mafanikio yake
[hariri | hariri chanzo]Msimu | Vipindi | Ilianza | Ilimalizika | Watazamaji (in milioni) |
Namba | |
---|---|---|---|---|---|---|
1 | 2003-2004 | 25 | 23 Septemba 2003 | 14 Mei 2004 | 8.23[1] | |
2 | 2004-2005 | 26 | 24 Septemba 2004 | 6 Mei 2005 | 6.94[2] | |
3 | 2005-2006 | 22 | 30 Septemba 2005 | 2 Mei 2006 | 5.8[3] |
Wahusika Wakuu
[hariri | hariri chanzo]- Hope Fairfield-Shanowski (Faith Ford). Hope ndiye mama wa familia. Ameolewa na Charley na ana watoto watatu: Sydney, Haley, na Justin. Anapenda kupika na kupanda miti kwenye bustani lake.
- Faith Fairfield (Kelly Ripa). Faith ni nduguye Hope. Yeye ni mvivu, na anamfanya Hope amtendekeze. Mara kwa mara, anazua vitimbi na kumshirikisha nduguye. Yeye amejaribu kutafuta kazi kama mwigizaji, lakini hakufaulu.
- Charley Shanowski (Ted McGinley). Charley ni mumewe Hope. Yeye hampendi Faith, na kila mara anajaribu kumfukuza Faith kwenye nyumba. Yeye ni daktari wa meno na anapenda kuangalia michezo.
- Sydney Shanowski (Nicole Paggi). Sydney ni mtoto wa kwanza wa Hope na Charley. Yeye anampenda Faith zaidi ya mamake.
- Hayley Shanowski (Macey Cruthird). Hayley ni mwana wa pili wa Hope na Charley. Ni mtoto mwerevu aliyerukishwa hadi darasa la kidato cha pili. Yeye ni mwenye huruma na anapenda wanyama.
- Justin Shanowski (Jansen Panettiere). Ni mwana wa mwisho. Ni mtoto mwerevu anayempenda babake na Faith sana.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Viewership numbers of primetime programs during the 2003-04 television season". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-02-08. Iliwekwa mnamo 2010-01-28. Retrieved on 2007-11-06.
- ↑ "Season Program Rankings from 09/20/04 through 05/22/06". ABC Medianet. 24 Mei 2005. Iliwekwa mnamo 2009-07-03.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-12-08. Iliwekwa mnamo 2006-12-08.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help); Unknown parameter|https://web.archive.org/web/20061208201731/http://www.hollywoodreporter.com/hr/search/article_display.jsp?vnu_content_id=
ignored (help)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Hope & Faith katika Internet Movie Database