Nenda kwa yaliyomo

Hifadhi ya taifa ya Milima ya Simien

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ethiopia, Gondar
Hifadhi ya taifa ya Simien

Hifadhi ya taifa ya Milima ya Simien, ndiyo mbuga kubwa zaidi ya taifa nchini Ethiopia . Iko katika Ukanda wa Kaskazini wa Gondar, Mkoa wa Amhara.

Ni makazi ya spishi kadhaa zilizo hatarini kutoweka, kama vile mbwa mwitu wa Ethiopia na walia ibex, mbuzi-mwitu ambaye hapatikani kwingine popote duniani. Nyani aina ya gelada na caracal, paka, pia hutokea ndani ya Milima ya Simien. Zaidi ya aina 50 za ndege hukaa katika hifadhi hiyo [1]

Hifadhi hiyo inavukwa na barabara isiyo na lami ambayo inatoka Debarq, ambapo makao makuu ya hifadhi yapo, mashariki kupita vijiji kadhaa hadi mita 4,430, ambapo barabara inageuka kusini hadi mwisho huko Mekane Berhan, kilomita 10 nje ya mpaka wa hifadhi. [2]

Picha katika hifadhi

[hariri | hariri chanzo]


  1. WordTravels Ethiopia Travel Guide Ilihifadhiwa 1 Desemba 2017 kwenye Wayback Machine., Retrieved on June 22, 2008
  2. Philip Briggs, Ethiopia: The Bradt Travel Guide, 5th edition (Chalfont St Peters: Bradt, 2009), p. 240
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya taifa ya Milima ya Simien kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.