Nenda kwa yaliyomo

Hifadhi ya Msitu wa Atewa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hifadhi ya Msitu wa Atewa, iko katika eneo la Akyem Abuakwa kusini mashariki mwa Ghana, karibu na mji wa Kibi, na kusini magharibi mwa Uwanda wa Kwahu ambao unaunda mpaka wa kusini-magharibi wa Ziwa Volta.

Hifadhi ya Msitu[hariri | hariri chanzo]

Giant African swallowtail ( Papilio antimachus )

Eneo kubwa la hifadhi hiyo limetangazwa kuwa hifadhi ya msitu, Likijumuisha takribani hekta 17,400 za msitu wa kijani kibichi, ambao ni nadra katika nchi ya Ghana.

Hifadhi hiyo inasimamiwa na Tume ya Misitu ya Ghana kwa ushirikiano na wadau wengine, muhimu miongoni mwao ni Taasisi ya Mazingira ya Okyeman, ambayo imewazuia watu kulima katika eneo hilo na badala yake inajaribu kuhimiza utalii wa mazingira. [1] Hata hivyo, hifadhi iko chini ya shinikizo la ukataji miti na kuwinda nyama ya porini. Pia ni hatari kwa shughuli za uchunguzi wa madini, kwa kuwa hifadhi hiyo ina madini ya dhahabu pamoja na bauxite ya kiwango cha chini. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Eco - Fest Foundation at Atewa Range", Biodiversity Reporting Award, June 2001. Retrieved on 2009-03-20. Archived from the original on 2010-12-13. 
  2. "Study of Pristine Ghanaian Forest reveals new, rare and threatened species". Wildlife Extra. Desemba 2007. Iliwekwa mnamo 2009-03-20.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)