Hendrick Witbooi
Hendrick Witbooi, kwa jina asilia ǃNanseb ǀGabemab (1840 - 1905) alikuwa chifu wa kabila la Nama katika Namibia ya leo, kiongozi wa mapambano dhidi ya ukoloni wa Kijerumani na mwandishi.
Alizaliwa katika jimbo la rasi la Afrika Kusini akalelewa kama Mkristo. Mnamo 1855 alihamia pamoja na kabila lote Namibia. Alikuwa mtoto wa chifu wa awali akapokea uongozi kutoka kwa baba.
Katika miaka ya 1880 aliunganisha makabila yote ya Wanama chini ya uongozi wake na tangu 1890 aliingia katika mapambano na wakoloni Wajerumani. Baada ya kushondwa mara ya kwanza alipatana amani lakini wakati wa vita ya Wajerumani dhidi ya Waherero alijiunga nao. Mwaka wa 1905 alikamatwa na kuuawa na Wajerumani.
Shajara yake aliyoiandika kwa lugha ya Kiholanzi ilitolewa mwaka wa 1929 tu.
Maandishi yake
[hariri | hariri chanzo]- Die Dagboek van Hendrick Witbooi, Kaptein van Witbooi-Hottentotte, 1884-1905 (1929, baada ya kifo chake)
Angalia pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Chapman, Michael. 2003. Southern African Literatures, University of Natal Press. ISBN 1-86914-028-1
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hendrick Witbooi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |