Hawa Mayoka Said
Hawa Mayoka Said | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Majina mengine | Hawa |
Kazi yake | Mwimbaji |
Hawa Mayoka Said (watu wengi wanamjua kama Hawa) ni mwimbaji ambaye anatokea Tanzania.
Maisha ya utotoni
[hariri | hariri chanzo]Hawa anaishi Dar es Salaam, Tanzania. Mama yake anaitwa Ndagina Hassan. Hawa ana mtoto mmoja.
Hawa aliimba na Diamond Platinumz wimbo ambao unaitwa “Nitarejea[1]”, mwaka wa 2011. Watu wengi waliupenda wimbo huo na wanaamini kwamba wimbo huo ulimpa Diamond Platinumz umaarufu na manifikio. Lakini Hawa hakupata umaarufu au manifikio kama Diamond Platinumz. Baada ya huo wimbo, Hawa hakuweza kutoa wimbo mwingine Archived 26 Julai 2019 at the Wayback Machine.[2].
Ndoa
[hariri | hariri chanzo]Mwaka wa 2015, Hawa aliolewa lakini ndoa yake haikukaa kwa muda mrefu. Ndoa yake ilivunjika baada ya miezi kama nne Archived 26 Julai 2019 at the Wayback Machine.[3]. Mume wake alimwacha na alimwambia kuwa angerejea nyumbani baada ya muda mfupi. Alisema kuwa alikuwa anaenda kwa kazi yake. Lakini hakurudi. Baada ya mume wake kumwacha, Hawa alianza kunywa pombe na kuvuta sigara sana.
Ugonjwa
[hariri | hariri chanzo]Mwezi wa saba mwaka wa 2018, Hawa alikuwa mgonjwa sana na madaktari wa Tanzania walimwambia ana miezi michache tu ya kuishi. Hata hivyo walimshauri ajaribu kuenda nchi ya India kutafuta matibabu. Lakini Hawa hakuwa na pesa za kuenda nchi ya India. Hawa hakuwa na tumaini na maisha yake kwa sababu hakujua kama angeweza kupata pesa za kuenda nchi ya India kwa matibabu. Hawa na mashabiki walimwomba Diamond msaada ili Hawa aweze kutibiwa na madaktari. Diamond aliahidi kuwa atampa. Diamond alilipia matibabu yote na usafiri kuenda nchi ya India. Hawa alifurahi sana baada ya kusikia habari hizo. Hatimaye, Diamond alimtumia kama shilingi millioni 50 Archived 26 Julai 2019 at the Wayback Machine.[4].
Tarehe 13 Oktoba 2018 Archived 26 Julai 2019 at the Wayback Machine.[5], Hawa na mama yake walijaribu kuenda nchini India baada ya kupata msaada kutoka kwa Diamond lakini walirudishwa kutoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa mji wa Dar es Salaam kwa sababu Hawa hakuwa na karatasi ya daktari ambayo ilionyesha ugonjwa wake. Baada ya kupata karatasi ya daktari, meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz, alikwenda na Hawa na mama yake ili kuwasaidia. Hawa apolifika nchini India, madaktari walisema kuwa hakuwa na ugonjwa wa ini lakini alikuwa na tatizo la moyo Archived 26 Julai 2019 at the Wayback Machine.[6]. Walisema kuwa alihitaji utaratibu mkubwa wa upasuaji ili kusuluhisha tatizo la moyo wake. Upasuaji wa Hawa ulikua upasuaji wa mafanikio.
Mipango ya baadaye
[hariri | hariri chanzo]Hawa alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kurudi katika hali yake ya kawaida, na bila kumsahau Diamond Platnumz aliyefanikisha hilo. Diamond aliandika kwenye ukurasa wake (Intagram) haya maneno Archived 26 Julai 2019 at the Wayback Machine.[7] “Nafarijika kuona unatabasamu sasa nitafurahi kusikia wazo zuri la biashara toka kwako nikuwezeshe.” Sasa hivi Hawa ana afya nzuri na anamshukuru Mungu sana na ana mipango ya kurudi kufanya muziki tena. Yeye alisema kuwa ana vitu vingi vya kuwaambia Watanzania. Hawa alirudi Tanzania baada ya matibabu yake na aliwashukuru Watanzania kwa maombi na msaada wao, muhimu zaidi alimshukuru Diamond kwa msaada aliompa wakati alipokuwa mgonjwa sana. Hawa anaamini kuwa vitu vyote vitakuwa salama kwa sababu Mungu yuko pamoja naye. Sasa Hawa ana matumaini kwa maisha yake.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ abdi d (2011-02-13), DIAMOND FT. HAWA - NITAREJEA- (Official Video), iliwekwa mnamo 2019-07-26
- ↑ "Hawa of 'Nitarejea' reveals how she met with Diamond Platnumz – Daily Active Kenya" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-26. Iliwekwa mnamo 2019-07-26.
- ↑ "Masaibu! Diamond Platnumz's Alleged Baby Mama And Bongo Singer Wallowing Away In Alcohol And Tobacco Addiction". Classic 105 (kwa American English). 2017-07-19. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-26. Iliwekwa mnamo 2019-07-26.
- ↑ hot96user (2018-10-15). "Ailing Hawa of 'Nitarejea' stopped from leaving Tanzanian airport for India". Hot 96 (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-26. Iliwekwa mnamo 2019-07-26.
{{cite web}}
:|author=
has generic name (help)CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ "Ailing Hawa of 'Nitarejea' stopped from leaving Tanzanian airport for India". eDaily Kenya (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-26. Iliwekwa mnamo 2019-07-26.
- ↑ "Not liver-related complications: Hawa of 'Nitarejea' diagnosed with different disease in India". eDaily Kenya (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-26. Iliwekwa mnamo 2019-07-26.
- ↑ "Diamond to sponsor Hawa's business after her return from India – Daily Active Kenya" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-26. Iliwekwa mnamo 2019-07-26.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hawa Mayoka Said kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |