Nenda kwa yaliyomo

Harold Lloyd

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Harold Lloyd - Aug 1922 Photoplay.

Harold Clayton Lloyd (20 Aprili 1893 – 8 Machi 1971) alikuwa mchekeshaji maarufu wa filamu za kimya kutoka nchini Marekani. Baba yake alikuwa James Darsie Lloyd na mama yake Milly Rapp. Lloyd alijulikana kwa ucheshi wake wa kipekee na matukio ya hatari aliyoyafanya mwenyewe, akiwa na ushawishi mkubwa katika historia ya filamu nchini Marekani.

Lloyd alianza kazi ya uigizaji mwanzoni mwa karne ya 20. Aliingia kwenye tasnia ya filamu mwaka 1913 na kuanza kupata umaarufu kutokana na vipaji vyake vya uigizaji na ucheshi. Alicheza nafasi mbalimbali katika filamu za kimya kabla ya kugundua mtindo wake wa kipekee uliomhusisha kuwa na tabia ya "The Glasses Character," akitumia miwani kama alama ya utambulisho.

Alicheza katika filamu nyingi maarufu kama "Safety Last!" (1923), ambapo alionekana akipanda mnara wa saa, na "The Freshman" (1925), filamu iliyozungumzia maisha ya mwanafunzi wa chuo kikuu. Uwezo wake wa kuunganisha ucheshi na matukio ya hatari ulimfanya awe mchekeshaji wa aina yake. Katika harakati za kujipatia riziki, alipata ajali mwaka 1919 wakati wa kuchukua picha, ambapo kifaa cha baruti kililipuka na kumjeruhi. Hali iliyopelekea kupoteza kidole gumba na cha pili cha mkono wake wa kulia. Licha ya tatizo hili, aliendelea na kazi yake na kujipakulia mafanikio zaidi.

Filamu zake

[hariri | hariri chanzo]
Namba Jina la Filamu Mwaka Mwongozaji
1 Safety Last! 1923 Fred C. Newmeyer, Sam Taylor
2 The Freshman 1925 Fred C. Newmeyer, Sam Taylor
3 Girl Shy 1924 Fred C. Newmeyer, Sam Taylor
4 Speedy 1928 Ted Wilde
5 The Kid Brother 1927 Ted Wilde
6 Why Worry? 1923 Fred C. Newmeyer, Sam Taylor
7 Grandma's Boy 1922 Fred C. Newmeyer
8 Dr. Jack 1922 Fred C. Newmeyer
9 Hot Water 1924 Fred C. Newmeyer, Sam Taylor
10 For Heaven's Sake 1926 Sam Taylor


Makala hii ni sehemu ya mradi wa kuboresha Wikipedia na Wikamusi ya Kiswahili. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari.