Hamisa Mobetto
| Hamisa Hasan Mobeto | |
| Amezaliwa | 10th December 1994 Mwanza |
|---|---|
| Nchi | Tanzania |
| Kazi yake | Mwimbaji, mwanamitindo |
Hamisa Hassan Mobetto (alizaliwa Mwanza, Tanzania, Disemba 10, 1994)[1] ni mwimbaji, mwigizaji, mfanyabiashara, na mwanamitindo wa Tanzania.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa katika familia ya Kiislamu na alikuwa na shauku ya uanamitindo akiwa mtoto.
Aliendeleza kazi yake katika uana mitindo baada ya kumaliza shule ya sekondari.[2]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Urembo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka 2011, alishiriki katika mashindano ya uzuri ya Miss Indian Ocean 2011, ambapo alishika nafasi ya pili ya pili (2nd runner up). Mwaka huo huo, nafasi yake ya pili ilimfanya kushiriki katika Miss Tanzania 2011. Mnamo 2012, alishiriki katika Miss University Africa na kufanikisha kufika miongoni mwa washiriki 10 bora.
Mnamo 2017, aliteuliwa kwa Tuzo ya People's Choice Award na Super Mum katika Starqt International Awards.
Mnamo 2018, alishinda tuzo ya Female Stylish Of The Year katika Swahili Fashion Week Awards. Mwaka huo huo, aliteuliwa kuwa mgeni rasmi (host) wa Miss Tanzania Beauty Pageant. Mwaka huo huo pia aliteuliwa kwa Tuzo ya Best East African Woman Entrepreneur katika BEFFTA Awards.
Mnamo Desemba 2020, alishinda tuzo ya Best Female Digital Model of the Year katika Tanzania Digital Awards.
Muziki
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 2017, Hamisa alionekana kwenye video na Diamond Platnumz kwenye wimbo maarufu wa "Salome".
Mnamo 2018, alitoa wimbo wake wa kwanza rasmi ulioitwa "Madam Hero". Wimbo huu ulimtambulisha katika tasnia ya Bongo Flava na kufikia maoni zaidi ya milioni mbili kwenye YouTube. Mwaka huo huo pia alitoa wimbo "Tunaendana".
Mnamo 2021, alizindua lebo yake ya muziki, Mobetto Music.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Dennis Milimo (2019-03-27). "Hamisa Mobetto exposed for lying about her real Age". Pulselive Kenya (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-05.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-05-05. Iliwekwa mnamo 2024-05-05.
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hamisa Mobetto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |