Hadj Bouchiba
Hadj Bouchiba (1903 – Januari 5, 1957)[1] alikuwa mwandishi wa nyimbo, mtunzi, mshairi na mchoraji.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Abdelghani Bouchiba alizaliwa Constantine, Algeria mwaka 1903 ila alihamia Algiers akiwa katika umri mdogo pamoja na baba yake Salah aliyekuwa na maduka mawili ya viatu zenye staili za kiarabu huko Casbah. Mwaka 1923 aliishi na wazazi wake Rampe Valée. Aliitwa kuhudumu katika jeshi kisha kupata kazi yake ya kwanza kama fundi na kisha kuwa dereva wa mashine. Baada ya kumaliza kuhudumu jeshi, Bouchiba alijikita zaidi katika muziki kuanzia mwaka 1924 mpaka 1925. Baada ya mwonekano wa mwanzo katika medh chaabi taratibu Bouchiba alichagua El Arrobi ambayo ingepelekea kumpeleka katika ngazi ya juu na iliwavutia watu wa Fahs ambapo Bouchiba alipopata mahali pa kudumu. Januari 5, 1957 Bouchiba alipigwa risasi na La Main Rouge, shirika la siri la kikoloni. Alizikwa katika makaburi ya El Kettar.
Nyimbo
[hariri | hariri chanzo]- Mahl El Djoudi
- Ya akhina[2]
- .Ya Doukar Edjnani
- Sbouhi
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Culture : AYANT EU DE NOMBREUX ADEPTES Le chaâbi entre histoire et théorie". Le Soir d'Algérie. Machi 9, 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 7, 2014. Iliwekwa mnamo Aprili 2, 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ performed by Kamel Bourdib