Giza (Misri)
Mandhari
Giza | |||
| |||
Mahali pa mji wa Giza katika Misri |
|||
Majiranukta: 30°01′0″N 31°13′0″E / 30.01667°N 31.21667°E | |||
Nchi | Misri | ||
---|---|---|---|
Mkoa | Giza | ||
Idadi ya wakazi | |||
- Wakazi kwa ujumla | 2,443,490 |
Giza (pia: Gizeh, kutoka Kar.: الجيزة al-gīza) ni mji wa kaskazini ya Misri unaopakana na mji mkuu Kairo. Kuna wakazi 2,443,490 (2005).
Mji wa Giza waonekana kama mtaa wa Kairo tu lakini ni mji wa pekee. Zamani ilitengwa na mji mkuu kwa uwazi wa mashamba lakini siku hizi miji yote miwili imekua hadi kugusana kabisa.
Giza yajulikana hasa kama mahali pa piramidi.