Girls Like Us

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Girls Like Us
MudaDakika 3 na Sekunde 25
Kampuni ya utayarishajiActuality Media, LLC
Imeongozwa naC. Dallas Golden
Imetayarishwa naHailey Sprinkel
NyotaWinnie Msamba
Imehaririwa naKate McCallum
Muziki naFollow your heart na wind of hope from audioblocks.com na Ricky Valadez kutoka pond5.com
SinematografiaJeffrey Rodriguez
NchiTanzania
LughaKingereza

Girls Like Us ni filamu / video fupi iliyotengenezwa mwaka 2016 ikiongozwa na Pond Ripple Media, LLC, yenye kuyaangazia maisha ya binti wa Kitanzania mwenye ndoto za kufika mbali kimaisha[1] ilhahi anatokea kwenye familia ya kawaida yenye mama, baba, dada, kaka na kuzungukwa na ndugu wengine. Filamu hii fupi inamuhusu Winnie Etmas Msamba binti ambaye tangu akiwa na umri mdogo alikuwa na ndoto kubwa. Pia filamu hii fupi inaelezea na kuonesha umuhimu wa kuwa na watu wa kuwatizama katika maisha ambao watakuongoza katika njia iliyo sahihi ili kuweza yafikia malengo yako.

Mwanzo wa filamu[hariri | hariri chanzo]

Filamu inaanza kwa kuonesha mazingira ya mtaani nyumbani kwa kina Winnie. Mazingira haya ni mazingira ambayo asilimia kubwa ya wanafunzi wa rika la Winnie Msamba na wenye kusoma shule za Kata au shule za serikali wanatokea. Ni mazingira yenye nyumba zisizo na Fenzi, na kama fensi ipo basi ni fupi kiasi na majirani hususani vijana hupenda kukaa nje wakipigwa na upepo.

Kama mabinti wengine wakitanzania walivyo, inawapasa kufanya kazi kabla ya kuondoka nyumbani, ndivyo inavyo oneshwa katika filamu hii huku Winnie akiandaa Jiko kwa ajili ya mapishi ya wakati huo. Tunavushwa mpaka muda wa Winnie kuondoka akiwa amebeba begi na kuvalia nguo za nyumbani.

Huu ni wakati wa likizo ya kusubiria matokeo ya kidato cha nne, ni Muda ambao Winnie ameamua kujitolea kufanya shughuri za Taasisi ya Apps and Girls. Yupo kama mwanafunzi na Mentor kwa wanafunzi wa shule za secondary ikiwemo shule ya Jangwani.[1]

Wahusika na wasifu wao wa nje[hariri | hariri chanzo]

  1. Winnie Msamba: Huyu ni mhusika mkuu. Filamu hii fupi inahusisha njia alizo pita na kuonesha anako tamani kuelekea. Nje ya Filamu hii Winnie Msamba hajabadirisha ndoto zake. Kama ilivyo katika filamu hii, aliweza kufanikisha ndoto yake na kuweza fanikiwa maliza masomo yake katika Shule ya African Leadership Academy nchini Africa Kusini na kuweza endelea na Masomo Nchini Marekani na Kenya. zaidi ya kumaliza masomo Winnie ameshirikiana na wenzake na kuanzisha Kampuni iitwayo Africa Harvest Enterprises (T) Limited, [2]Katika kutimiza ndoto zake Winnie Msamba ni mmoja wa wanufaika wa program za Jeff Bezzos zenye kuwanufaisha vijana wadogo kuweza timiza ndoto zao kwa kuwapa maarifa na kuweza wakutanisha na watu wakubwa wenye ushawishi katika biashara.[3]
  2. Carolyne Ekyarisiima: Ni mshiriki katika filamu hii. Amehusika kuonesha namna mabinti wanaweza tafuta watu wa kuwaongoza japo kwa uchache katika kutimiza ndoto zao. Winnie Msamba alipo kutana na Carolyne Ekyarisiima[4] akatamani kuwa karibu naye. Ajifunze ili aweze kuwa bora na kuweza timiza ndoto zake kama wanawake wengine katika jamii wenye vyeo na mafanikio makubwa kibiashara. Carolyne ni mjasiriamali jamii, mwanasayansi na mfanya biashara, mwanzilishi wa Taasisi ya Apps and Girls yenye kuwasaidia mabinti kutambua uwezo wao, kuweza kuwaza kwa ukubwa, kuota ndoto kubwa na kuweza simama imara katika kufanikisha ndoto hizo.
  3. Necta Richard: Ni mhusika aliye onesha uhitaji wa kuwa na mtu wa kukupa moyo pale unapo angua iwe ni mara moja au zaidi ya moja. Kushiriki kwake katika mashindano na kushindwa kumalizia kuwasilisha wazo lake kulimfanya aamini ule ndio ulikuwa mwisho wake, uwepo wa Winnie Msamba katika wakati huo mgumu kwake ukampa faraja hasa baada ya kupewa maneno yaliyo mtia moyo kwamba yeye si wa kwanza kufeli[1]. Necta Richard ni Mwana Mwana TEHAMA mbobezi kwenye mambo ya kutengeneza program za kompyuta. Alikuwa mwanafunzi mwenye ndoto alipokuwa Jangwani[5] na mara baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari aliendelea na masomo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Mapokezi ya filamu[hariri | hariri chanzo]

Kwenye Mitandao ya Kijamii hasa kwenye mtandao wa Vimeo, Video au filamu ya "Girls Like Us" imetazamwa mara 2,265. Kwa Hapa Tanzania imetazamwa na wanafunzi wengi. Hii ni baada ya Taasisi ya Apps and Girls kuiweka katika CD na Flash na kuigawa kwa wanafunzi mashuleni ili itumike katika kuinua ari za kupenda kuota ndoto kubwa na zaidi kupenda masomo ya STEM.

Teuzi na Tuzo mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

  1. 1st Place for The MY HERO Award chini ya Category ya Haki za Wanawake (2017) By The MY HERO Project (Ilishinda)
  2. 2017 Awareness Festival in Los Angels (Ilipendekezwa)[6]
  3. Zlatna International Ethnographic Film Festival 2017 (Ilipendekezwa)
  4. Impact Film Festival, Washington, D.C (Ilipendekezwa)
  5. Show Me Justice Film Festival 2017 (Ilipendekezwa)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 Abroad, Actuality (2016-09-22), Girls Like Us, iliwekwa mnamo 2024-02-06 
  2. "Africa Harvest Enterprises (T) Limited". VC4A (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-02-06. 
  3. "Scholar Spotlight: Winnie Godlove Msamba, 2017 Bezos Student Scholar | Bezos Scholars Program". www.bezosscholars.org. Iliwekwa mnamo 2024-02-06. 
  4. https://dotrust.org/my-advice-use-the-resources-you-already-have/
  5. Mtanzania Digital (2016-07-15). "NECTA RICHARD: Nataka kuwa mhandisi kuisaidia nchi yangu". Mtanzania (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2024-02-06. 
  6. "Awareness Festival – Films That Do More Than Entertain" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2024-02-06.