Nenda kwa yaliyomo

Georgetown, Guyana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Georgetown, Gayana)


Jiji la Georgetown
Nchi Guyana
Jengo la Bunge la Guyana mjini Georgetown

Georgetown ni mji mkuu wa Guyana na mji mkubwa wa nchi hii ya Amerika Kusini. Ina wakazi 32,563 mjini penyewe na 134,599 pamoja na rundiko la mji.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mji ulianzishwa na Wafaransa mnmao mwaka 1782 kwa jina la Longchamps ("shamba ndefu") na baadaye "La Nouvelle Ville" ("mji mpya"). Mji ulikabidhiwa kwa Uholanzi mwaka 1784 kama sehemu ya Guyana ya Kiholanzi na kuitwa "Stabroek".

Wakati wa vita za Napoleoni Uholanzi ilivamiwa na Ufaransa na Uingereza kama adui wa Napoleon ilikamata koloni za Uholanzi. Hivyi mji ulikuwa chini ya utawala wa muda wa Uingereza na kupokea jina la Georgetown kwa heshima ya mfalme George III wa Uingereza na Hanover tangu 1812.

Mji pamoja na sehemu za karibu za Guyana ya Kiholanzi zilihamishwa kikamilifu chini ya utawala wa Uingereza tangu 1814 na kuwa Guyana ya Kiingereza.

Leo hii Georgetown ni kitovu cha utawala na uchumi wa nchi ya Guyana. Kuna ofisi za serikali, bunge, mahakama, chuo kikuu na bandari.

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Georgetown, Guyana kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.