Gemma Sisia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Gemma Sisia
Amezaliwa3 Novemba 1971 (1971-11-03) (umri 49)
UtaifaMuaustralia
CheoMuasisi wa shule ya St Jude
Watoto4

Gemma Sisia (jina la kuzaliwa Gemma Rice;[1] alizaliwa 3 Novemba 1971[2]) ni mfadhili kutoka Australia.

Mwaka 2002 alianzisha Shule ya St Jude iliyopo Tanzania,[3] shule ambayo inatoa elimu bure na ya kiwango bora kwa watoto wa Tanzania zaidi ya 1,800; kati yao zaidi ya 1,400 wanalala bwenini."[4]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Sisia amekulia huko Armidale, New South Wales|Armidale, Australia katika shamba la familia ambapo walikuwa wanajishughulisha na ufugaji wa kondoo wa sufu.[2][5] Ni binti pekee katika familia yenye watoto nane.[2] Mama yake mzazi anafahamika kwa jina la Sue na baba mzazi anafahamika kwa jina la Basil Rice.[2] Katika utoto wake , Gemma alishindana kwenye urushaji farasi.[6] Alihitimu elimu ya juu chuo cha St Vincent (St Vincent's College, Potts Point|St Vincent's College).[3][7] Familia yake ilisisitiza sana juu ya elimu wakati akikua.[8]

Katika masomo yake ya chuo huko University of Melbourne|Melbourne University, Gemma alibobea katika masomo ya biochemistry, genetics, na elimu.[8] Akiwa na umri wa miaka 22, alihamia Uganda kufanya kazi katika shule ya wahudumu.[8] Ambapo miezi michache baadaye alipotembelea Tanzania, alikutanan na Richard Sisia, dereva wa safari wa kitanzania.[8] Wawili hao baadae walioana na kufanikiwa kupata watoto wanne.[8]

Gemma alifungua shule ya St Jude mnamo januari 2002.[8] Kwa sasa shule hyo imekua na kufikia idadi ya wanafunzi wapatao 1,800,[9] wanafunzi wote hupata elimu bora na ya bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari."[5] Shule pia ilianzisha program maalumu kwa ajili ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita, program hyo ilianza rasmi mwaka 2015 baada nya wahitimu wa kwanza kumaliza masomo ya sekondari. Kabla ya kuendelea na masomo ya chuo kikuu, wanafunzi hao hushiriki kwa hiari katika huduma ya kujitolea, mara nyingi kwa kufundisha katika shule za uma.[10]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gemma Sisia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.