Flavour
Chinedu Okoli (anajulikana zaidi kwa jina la kisanii Flavour N'abania au kwa kifupi Flavour; alizaliwa Jimbo la Enugu, 23 Novemba 1983) ni mwimbaji wa Nigeria.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Flavour, anayejulikana kwa uwezo wake wa kuimba kwa ufasaha katika Lugha ya Kiigbo,[1] alizaliwa katika eneo la kusini mashariki mwa Nigeria. Asili ya familia yake ni kutoka Umunze katika Halmashauri ya Serikali za Mitaa ya Orumba South, Jimbo la Anambra, kusini mashariki mwa Nigeria.[2] Flavour alianza taaluma yake ya muziki akiwa na umri wa miaka 13, alipokuwa akiimba nyimbo za kwaya katika kanisa allokua akisalia mjini Enugu, Jimbo la Enugu. Mchungaji wa kanisa lake alimjulisha kwa rafiki yake, Chris I. Ordor, Mkurugenzi Mtendaji wa SoundCity Communications. Mwaka wa 1996, Flavour alialikwa kujiunga na kampuni hiyo kupitia ufadhili wa masomo ili kusomea muziki.
Baada ya miaka mitatu ya kupiga ngoma, Flavour alianza kupiga ngoma kitaalamu. Mnamo 1999, aliacha kupiga ngoma na kuanza kupiga kinanda.[3] Pia aliwahi kutoa sauti za nyuma kwa wasanii wengine katika SoundCity.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Flavour basking on longevity and originality with Igbo highlife". 18 Machi 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 29 Machi 2021.
- ↑ "Tovuti Rasmi ya Flavour N'abania". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Aprili 2012. Iliwekwa mnamo 8 Novemba 2011.
- ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>tag; no text was provided for refs namedSun - ↑ "Chinedu Okoli". Igbo People Biography (kwa Kiingereza). IgboPeople.org. Iliwekwa mnamo 7 Mei 2025.
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Flavour kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |