Nenda kwa yaliyomo

Filamu za Kajal Aggarwal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kajal Aggarwal ni mwigizaji wa Kihindi ambaye mara nyingi huonekana katika filamu za T Kitelugu na Kitamil, pamoja na filamu za Kihindi. Alianza kucheza kama muhusika mdogo katika filamu ya Kihindi ya Kyun! Ho Gaya Na... (2004). Aggarwal alianza kazi yake katika sinema ya Telugu na Lakshmi Kalyanam (2007), ambayo haikuwa na mafanikio sana katika mapato. Lakini filamu nyingine ya Telugu ya mwaka huohuo, Chandamama, ilikuwa mafanikio makubwa kibiashara.[1]Filamu yake ya kwanza ya Tamil, Pazhani, ilikuja mwaka uliofuata. Pia mwaka mwingine uliofata alikuwa na filamu nne. Moja wapo, filamu ya Telugu ya S. S. Rajamouli ya Magadheera, ilikuwa hatua kubwa kwake, [2]na ilimpatia uteuzi wa Tuzo ya Filmfare kwa Mwigizaji Bora - Telugu. Uzinduzi wa kwanza wa Aggarwal wa mwaka 2010 ulikuwa katika tamthilia ya mapenzi ya Darling, ambayo ilikuwa mafanikio makubwa kibiashara, na ilimpatia uteuzi mwingine wa Filmfare kwa Mwigizaji Bora - Telugu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Kajal: Flying high", The Times of India, 2008-06-17, ISSN 0971-8257, iliwekwa mnamo 2024-03-07
  2. "AN AVERAGE FARE". The Indian Express (kwa Kiingereza). 2010-07-16. Iliwekwa mnamo 2024-03-07.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Filamu za Kajal Aggarwal kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.