Nenda kwa yaliyomo

Encyclopedia Iranica

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Encyclopædia Iranica)

Encyclopædia Iranica ni kamusi elezo ya kitaalamu kuhusu historia, utamaduni, na ustaarabu wa watu wa Iran.

Ilianzishwa mwaka 1973 na profesa Ehsan Yarshater ikisimamishwa na taasisi ya Center for Iranian Studies kwenye Chuo Kikuu cha Columbia mjini New York.

Kamusi elezi hiyo inalenga kukusanya elimu ya kitaaluma kuhusu Iran wa leo lakini pia kuhusu maeneo yote yaliyokuwa sehemu za dunia ya Kiajemi katika historia. na uhusiano baina ya Uajemi na tamaduni nyingine kama vile China na Ulaya.[1] [2] Mradi unapanga kuchapisha jumla ya majuzuu 45 lakini tangu mwanzo maudhui yote inapatikana pia katika intaneti kupitia tovuti iranicaonline.org.

  1. Boss, Shira J. (Novemba 2003). "Encyclopedia Iranica". Columbia College Today. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-18. Iliwekwa mnamo 2016-07-14.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Trompf, Garry W. (2008). "Encyclopedia Iranica - 35: A New Agenda for Persian Studies?". Iran & the Caucasus. 12 (2): 385–395. doi:10.1163/157338408X406137. JSTOR 25597382.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]