Elvis Musiba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Aristablus Elvis Musiba (4 Februari 1950 - 31 Oktoba 2010) alikuwa mtunzi mashuhuri wa hadithi za kusisimua katika miaka ya 1980 kutoka nchini Tanzania.[1] Alivuma sana kwa tungo zake kama vile Kufa na Kupona, Kikomo, Kikosi cha Kisasi, Njama na Hujuma[2]. Musiba ni moja kati ya waandishi wa mwanzo nchini Tanzania kutunga hadithi za kijasusi, kipelelezi na kutisha. Hadithi ambazo baadaye zilipigwa topu. Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ufufuo mkubwa wa hadithi hizi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Vitabu vya Willy Gamba (Elvis Musiba) - JamiiForums (en-US). JamiiForums. Iliwekwa mnamo 2018-09-08.
  2. Mtunzi wa Willy Gamba, Elvis Musiba afariki dunia. Lukwangule Entertainment. Iliwekwa mnamo 2018-09-08.