Nenda kwa yaliyomo

Elizabeth Chijumba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ellizabeth Chijumba)


Elizabeth Chijumba
Alizaliwa 1982
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwigizaji, mwandishi na Muongoza filamu

Elizabeth Chijumba (maarufu kwa jina la "Nikita"; pia akijulikana kama "Fathia Chijumba", jina alilobadili baada ya kufunga ndoa na msanii mwenzake Khlafan maarufu kwa jina la Kevin [1]; alizaliwa 1982) ni mwanamke Mtanzania mwigizaji wa filamu za mapigano, pia mwandishi na mwongozaji wa filamu.

Baadhi ya filamu alizoigiza ni "Central Intelligent Department(CID)", Jumba la Dhahabu, The stolen Will akiwa na Steven kanumba pia katika filamu inayoitwa My Country.

Alisoma katika shule ya msingi ya Oysterbay jijini Dar-es-Salaam na baadae kuhamia katika shule ya msingi Mzumbe mkoani Morogoro [2].

Aliingia katika vinyang'anyiro vya mwandishi bora wa filamu na mwigizaji bora wa kike akibebwa na filamu ya "Copy" katika tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania [3]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elizabeth Chijumba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.