Nenda kwa yaliyomo

Ellen Thomas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ellen Thomas

Ellen Thomas (alizaliwa Januari 24, 1947) ni mwanaharakati aliyepigania kuwepo kwa amani nchini Marekani. Yeye alianza kujihusisha na mkesha wa amani ikulu inayotambulika (White House) mnamo Aprili 13, 1984. Binti wa mwanajeshi wa marekani, Thomas alizaliwa Brooklyn na kukua katika mji wa California. Alidhurika na silaha za nyuklia wakati wa utoto wake.[1] Katika kupinga sera za serikali ya Marekani, alipinga kodi kwa kuishi chini ya kiwango cha kodi ya mapato.[2]

Mnamo Mei 6, 1984, Ellen Benjamin aliolewa na Thomas katika harusi kubwa na kuitwa Ellen Thomas.[3] Thomas na mumewe waliandamana pamoja kwa miaka kadhaa, hadi kifo chake mnamo Januari 2009 kwa ugonjwa wa mapafu.

Ellen pia anaongoza "The Proposition One Non-Radioactive Nuclear Review", kikundi cha vyombo vya habari kinachosafiri kikielimisha umma juu ya hatari za siku zijazo za nyuklia. Mnamo 1993 alisaidia kuratibu mpango uliofaulu wa kura ya Washington DC kwa Upunguzaji wa Silaha za Nyuklia na mabadiliko ya Kiuchumi. Ellen alihudumu katika bodi ya wakurugenzi ya Washington Peace Center, lakini tangu wakati huo alihamia North Carolina. [4]

The Oracles of Pennsylvania Avenue (2012) kimeandikwa na Tim Wilkerson, filamu ya maandishi halisi iliyoidhinishwa na Al Jazeera Documentary Channel, inasimulia maisha ya William na Ellen Thomas, Concepción Picciotto na Norman Mayer. [5]

  1. Ellen Thomas
  2. Matt Hagengruber. "DC protest group stands test of time", KnightRidder, July 9, 2000. "I decided that when I didn't need to worry about providing for my daughter, I was going to reduce my income to below the poverty level so I wouldn't have to pay taxes, because I don't agree with the policies [of the US government]" 
  3. Birth of a street person by Lloyd Grove
  4. John Kelly (Novemba 6, 2011), "For 30-year peace activist, a new battle", The Washington Post, Ellen, who moved to the mountains of North Carolina after his [her husband's] death{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. The Oracles of Pennsylvania Avenue
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ellen Thomas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.