Nenda kwa yaliyomo

Ekwa Msangi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ekwa Msangi ni Mmarekani mwenye asili ya Tanzania, muandaaji wa filamu na mwandishi wa miswada ya filamu, pia ni anafundisha uandaaji wa filamu na masomo ya utamaduni katika Chuo Kikuu cha New York.[1][2]

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Msangi alizaliwa na wahamiaji mjini Oakland, California. Wazazi wake walikuwa wasomi wa Fulbright waliokuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha Stanford miaka ya 1980. Alikulia Kenya baada ya familia yake kuhamia huko alipokuwa na umri wa miaka mitano[2]

Mnamo Mwaka 1998, Msangi alikubaliwa kujiunga na Shule ya Sanaa ya NYU Tisch ambako alipata Shahada ya Kwanza ya Sanaa katika filamu na televisheni. Hapo awali akiwa amevunjika moyo na kuchanganyikiwa, mwelekeo wake ulibadilika baada ya kuchukua kozi iliyotolewa na mwanahistoria wa filamu za Kiafrika, Manthia Diawara. Alipata Shahada ya Uzamili (MA) katika sinema ya Kiafrika kutoka Shule ya Gallatin ya Masomo Binafsi katika chuo hicho hicho.[3]

Alianza kazi yake katika utayarishaji wa filamu, kisha akaendelea kutengeneza filamu fupi zilizoshinda tuzo kama vile vichekesho Soko Sonko (The Market King) na tamthilia za televisheni kwa vituo vya matangazo vya Kenya[4][5]. Filamu zake zimekuwa chaguo rasmi katika tamasha mbalimbali duniani ikiwemo Tamasha la Filamu la Kiafrika la New York na Tamasha la Kimataifa la Durban. Anajulikana zaidi kwa filamu yake ya Farewell Amor, iliyoonyeshwa kwa mara ya kwanza katika Tamasha la Filamu la Sundance la 2020 na kupata sifa kubwa kutoka kwa wakosoaji[6]

  1. "Ekwa Msangi". Vermont College of Fine Arts (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-11-27.
  2. 1 2 "Ekwa Msangi | Director, Writer, Producer". IMDb (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-08-24.
  3. "Ekwa Msangi". Vermont College of Fine Arts (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-08-24.
  4. "Tribeca Film Institute". www.tfiny.org. Iliwekwa mnamo 2025-08-24.
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-11-27. Iliwekwa mnamo 2025-08-24.
  6. Tambay Obenson (2020-02-06). "To Become an American Filmmaker, Ekwa Msangi Found Her African Voice". IndieWire (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-08-24.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ekwa Msangi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.