Eddy Kenzo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha Ya Mwanamuziki Eddy Kenzo
Picha Ya Mwanamuziki Eddy Kenzo

Edrisah Musuuza anajulikana kama Eddy Kenzo, ni mwimbaji na kutoka Uganda ambaye ni mwanzilishi na mwanachana wa Big Talent Entertainment. Alipata umaarufu kimataifa baada ya kuachiliwa kwa wimbo wake wa mwaka 2014, "Sitya Loss" na video inayoandamana ya mtandao ambayo iliangazia Ghetto Kids. Kwa ujumla ametoa albamu 4, ikiwa ni pamoja na Roots mwaka 2018 na hivi majuzi zaidi Made in Africa mwaka wa 2021. Kenzo pia ameshinda tuzo nyingi za kitaifa na kimataifa, zikiwemo Tuzo la Nickelodeon Kids' Choice mwaka wa 2018, Tuzo BET mwaka wa 2015 na nyingi. All Africa Music Awards.Alikuwa msanii wa kwanza wa Uganda kushinda tuzo ya BET mwaka 2015.

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Eddy Kenzo ambaye jina lake halisi ni Edrisah Musuuza alizaliwa[1] Masaka Uganda.Mama yake alifariki alipokuwa na umri wa miaka 4 au 5. Miaka 13 iliyofuata aliitumia zaidi akiishi katika mitaa ya Masaka na Kampala. Hapo awali Kenzo alitamani kuwa mwanasoka wa kulipwa na alijiunga na kambi ya Masaka Local Council FC's akiwa na umiri wa miaka 9. Baadae angepokea busari ya kuudhuria shule ya sekondari ya Lubiri mjini Kampala, lakini hakumaliza masomo yake[2]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Kenzo alianzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa kurekodi kutoka Uganda Rema Namakula. Mnamo 26 Desemba 2014, Rema Namakula na Eddy Kenzo walikuwa na binti katika hosipitali ya Paragoni, Kampala kitongoji cha Bugoloobi. Kenzo anaye binti mwingine (Maya Musuuza) kutoka kwenye mahusiano yake ya awali, alikubali yeye ndie baba na kumpa jina mtoto aliyezaliwa Amaal Musuuza[3]. Kenzo na Rema walitengana katikati ya mwaka 2019 na Rema mara moja akachumbiwa na daktari wake wa zamani Dkt. Hamza Ssebunya.[4][5][6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.cbc.ca/news/canada/toronto/eddy-kenzo-and-ghetto-kids-play-afrofest-1.4735844
  2. https://observer.ug/lifestyle/57579-why-eddy-kenzo-keeps-his-bet-award-at-the-museum
  3. http://matookerepublic.com/2014/12/27/kenzo-confirms-he-is-the-father-of-remas-baby-names-her-aamaal/
  4. https://www.newvision.co.ug/new_vision/news/1506765/rema-kenzo-wrong
  5. https://www.newvision.co.ug/new_vision/news/1506765/rema-kenzo-wrong
  6. https://www.independent.co.ug/kenzos-700-word-missive-to-rema/
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eddy Kenzo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.