Ekinokokasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka EKINOKOKASI)
Echinococcosis
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases, helminthologist Edit this on Wikidata
ICD-10B67.
ICD-9122.4, 122
DiseasesDB4048
eMedicinemed/629 med/1046
MeSHD004443

Ekinokokasi (maradhi ya hiadatidi) ni maradhi yenye kusababishwa na kimelea parasiti. Hiadatidi ni sisti za kiluwiluwi cha tegu “Taaenia echinococcus” masalia ya tishu za kiinitete Watu wanaumia aina mbili kuu ekinokokasi ya sisti na ekinokokasi alveolasi. Zaidi kuna aina mbili zingine zisizojulikana kama hizo ekinokokasi yenye sisti nyingi na ekinokokasi yenye sisti moja. Maradhi haya mara nyingi yanaanzia bila dalili huenda yanamudu muda wa mwaka katika hali hiyo. Dalili zilizopo zinategemea mahali panapo kuwa na sisti pamoja na ukubwa wao. Maradhi alveolasi kwa kawaida yanaumiza ini kwanza lakini yanaweza kusambaa hadi maeneo mengine ya mwili mifano mapafu au ubongo. Ini inapoathiriwa mgonjwa anaweza kupata maumivu ya fumbatio, ukosefu wa uzito, na umanjano yaani rangi yake ya manjano .. Maradhi ya mapafu huenda yanaletea kifua maumivu, kuhema upesiupesi, na kukohoa .[1]

Chanzo[hariri | hariri chanzo]

Maradhi haya yanasambaa kutokana na chakula au maji yenye mayai ya parasiti kuliwa, au kutokana na kukaribiana sana na mnyama anayeambukizwa.[1] Mayai huingia kinyesi cha wanyama wanaokula nyama nao wakaambukizwa na parasiti.[2] Wanaoambukizwa zaidi ni pamoja na mbwa, mbweha, na mbwa mwitu.[3] Ili wanyama hawa waambukizwe lazima wale ogani za mnyama mwenye sisti, Wa mifano ni kondoo au panya. Aina ya maradhi ambayo inaumiza binadamu inategemea na namna ya ekinokokasi inayosababisha uambukizo.[1]

Kwa kawaida uaguaji ni ya ultrisoni angalau tomografia ya tarakilishi au taswira za mwangwi mwenye sumaku huenda zinatumika.[4] Majaribio ya damu yatafutayo antibodi dhidi ya parasiti pengine yatasaidia kama ambavyo biopsi inaweza.[1] 

Ugangakinga na Matibabu[hariri | hariri chanzo]

Ugangakinga unaanzia kwa kutibu mbwa ambao pengine wameambukizwa pamoja na uchanjaji wa kondoo. Mara nyingi matibabu ni magumu. Maradhi ya sisti yanaweza kuondolewa kwa kupitia ngozi kukifuatiwa na dawa kutendewa. Mara nyingine aina hii ya maradhi inatazamwa tu. Aina ile ya alveolasi mara nyingi inahitaji upasuaji ukifuatiwa na dawa kutendewa. Dawa inayotumika ni “albandazole” ambayo huenda inahitajika kwa muda wa miaka.[3] Maradhi ya alveolasi yanaweza kuleta kifo.[1] 

Epidemiolojia[hariri | hariri chanzo]

Maradhi haya hutokea takribin sehemu zote za dunia. Siku hizi yanaumiza idadi ya watu milioni. Katika sehemu kadhaa za bara la Marekani ya Kusini pamoja na la Afrika, na la Asia hadi 10% ya idadi husika inaumizwa. Hadi 2010 vifo kutokana na maradhi haya yakawa 1200 upungufu kutoka 2000 mnamo mwaka wa 1990. Bei ya kiuchumi au kiasi uchumi unaopunguka thamani ni bilioni 3 kwa mwaka. Maradhi yanaweza kuambukiza wanyama wengine mifano ni nguruwe, ng’ombe na farasi. 

References[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Echinococcosis Fact sheet N°377". World Health Organization. March 2014. Iliwekwa mnamo 19 March 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "Echinococcosis [Echinococcus granulosus] [Echinococcus multilocularis] [Echinococcus oligarthrus] [Echinococcus vogeli]". CDC. November 29, 2013. Iliwekwa mnamo 20 March 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. 3.0 3.1 "Echinococcosis Treatment Information". CDC. November 29, 2013. Iliwekwa mnamo 20 March 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. "Neglected Tropical Diseases". cdc.gov. June 6, 2011. Iliwekwa mnamo 28 November 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)