Nenda kwa yaliyomo

Dr. Strange

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dr. Strange
Imetungwa na Greg Johnson
Hadithi:
Boyd Kirkland
Craig Kyle
Greg Johnson
Nyota Bryce Johnson
Imehaririwa na Aeolan Kelly
George Rizkallah
Imetolewa tar. Agosti 14, 2007 (2007-08-14)
Nchi United States
Lugha English

Doctor Strange: The Sorcerer Supreme ni filamu inayotokana na mhusika wa Marvel Comics Doctor Strange. Ilitolewa mnamo 14 Agosti 2007 na imepokea umaarufu kwa kuchezwa katika televisheni ya Cartoon Network ya Marekani mnamo 1 Novemba 2008.

Hii ni filamu ya nne iliyotiwa vibonzo iliyotayarishwa na Lionsgate ikihusiana na wahusika wa Marvel Comics, ikifuatia Ultimate Avengers, Ultimate Avengers 2 na The Invincible Iron Man.

Filamu hii inaangazia nguvu za kiuchawi na matukio ya kimiungu. Dr. Strange ambaye alikuwa Daktari wa upasuaji aliye na ujuzi mkuu ni mkaidi na hayajali mashauri ya wenziwe. Haonekani kuziamini nguvu za kichawi hadi anapokumbana na matukio ya ajabu anapoendesha gari kutoka kazini usiku.

Maa ya kwanza anachukulia mzaha anapoona Baron Mordo na wenziwe wakipigana na zimwi. Wakati huo huo anapaa habari kuwa watoto wa Daktari mwenzake Dk. Gina wanakumbwa na majinamizi na kuumwa na kichwa. Anapogusa mmoja anaona picha za mazimwi yale yale ya kutisha. Usiku huo anakumbana na masaibu yaleyale tena anapoendesha gari nyumbani, ambayo yanamanya kuhusika katika ajali mbaya akijaribu kuvihepa viumbe vilivyokuwa barabarani. Anapoteza mikono yake yote ambayo anatumia mali yak yote kuitibu akashindwa. Anaamua kujitoa uhai lakini Wong anamzuia na kumshauri amtafute mkale (Ancient One) kumfariji na kumponya kule Tibet.

Sephen anaanza mafunzo ya Ancient One ambaye ana wanafunzi wengine.

Kunaonekana kuwa na viumbe ambao wanaendelea kuwaua wanafunzi na siku inayofuatia, kuna mazimwi wawili na Mkale anamwamuru Baron Mordo kuwaua mmoja mmoja lakini anakaidi amri na matokeo ni wanafunzi wengi wengine kuyapoteza maisha. Mkale anamkashifu na kumwambia kuwa hangerithi nafasi ya ‘’Sorcerer Supreme’’ na badala yake aanze kumfunza strange ambaye angeirithi. Mordo anakasirishwa na kujaribu kumuua Strange ambay anasaidiwa na Wong. Wanagundua kuwa kuna zimwi Dormammu, ambalo linataka kutawala ulimwengu hasa dunia na linaingia duniani kupitia ndoto za watoto. Strange anarudi hospitalini kuwaamsha wagonjwa ili Dormammu asiwaingilie. Mordo pia anaingia mtoto anayelala kwa ndoto na kutengeneza mkataba na Dormammu amsaidie. Makabiliano makali yanafuatia kati ya Dormammu na Mordo dhidi ya Wong, Strange na Ancient One ambaye anaaga dunia. Vita vinabakia kati ya Dr. Strange ambaye ni Sorcerer Supreme mpya na Dormammu, lakini Strange anamshinda Filamu inaishia trange akimtembelea marehemu dadake katika kaburi na kuna habai za wanafunzi wapya wanaotaka kufunzwa na Strange, akiwemo msichana mdogo Clea.

Wahusika

[hariri | hariri chanzo]
Sauti Zingine

Upokeaji

[hariri | hariri chanzo]

Maoni kuhusu Doctor Strange: The Sorcerer Supreme yamekuwa yakichanganyika. Christopher Monfette wa IGN alisema filamu hii inacheza inavyotaajiwa na anamalizia kwa kusema, “utiaji vibonzo wa nguvu, uigizaji mzuri na upangaji mzuri wa wahusika unaifanya kuwa na uhai."[1]

Adam Arseneau wa DVD Verdict anaitaja filamu hii kuwa "imeshindwa kujenga masimulizi yake" na anaichongoa akisema inaisha kwa haraka kubwa lakini akasifu animation yake ya hali ya juu. [2].

Blake Matthews wa Blog Critics aliichambua akisema imepewa muda mchache sana wa Dakika 45 usioiruhusu kujenga hadithi ambayo inaanza kwa undani. Hata hivyo, anamalizia kwa kusema kuwa ilikuwa ya kuchekesha sana na mashabiki wangeifurahia[3].

Nick Lyons of DVD Talk anasema aliushtumu ubadilishaji wa mhusika lakini akasifu picha zake[4].

Marejeo kwa wahusika wengine wa Marvel

[hariri | hariri chanzo]
  • Wakati Stephen Strange anatoka hospitalini baada ya ajali yake, mwanamke anajitokeza Dk. Donald Blake (sura ya kibinadamu ya mungu wa radi) na anaonekana akitembea kupitia kwa mlango na mkongojo. Baadaye Dk. Blake anaonekana kama mmoja wa washauri ambao Strange anawatembelea kuhusu mikono yake.
  • Kuelekea mwisho ‘’Wong’’ anataja kuwa amepata mpiga ramli wa kike wa kutegemewa kwa jina la utani la Clea.
  1. DVD review Archived 2012-07-15 at Archive.today, Christopher Monfette, IGN, 7 Agosti 2007
  2. DVD review Archived 26 Machi 2010 at the Wayback Machine., Adam Arseneau, DVD Verdict, 24 Agosti 2007
  3. DVD review Archived 8 Oktoba 2008 at the Wayback Machine., Blake Matthews, Blog Critics, 24 Agosti 2007
  4. DVD review, Nick Lyons, DVD Talk, 8 Agosti 2007

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]