Nenda kwa yaliyomo

Donati Salla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ndg. Donati Salla (2014).

Donati Salla (alizaliwa katika kijiji cha Mkomongo, kata ya Kibosho Magharibi, Tarafa ya Kibosho, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro) ni mwanasiasa wa Tanzania.

Alisoma Elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Mkomongo Mnamo Mwaka 1996 - 2002.Alisoma Elimu ya Sekondari ya Kawaida katika Shule ya Sekondari Uru Mnamo Mwaka 2004 - 2007.↵Alisoma Elimu ya Juu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari Mwakaleli Mnamo Mwaka 2008 - 2010.

Alisoma na Kuhitimu Shahada ya Sanaa na Elimu (Elimu na Sosholojia) Katika Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agostino Tanzania Mnamo Mwaka 2010 - 2013.

Shughuli za Siasa

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Mwaka 2011 - 2012 alikuwa Katibu wa Wizara ya Huduma za Chakula na Afya Katika Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Stella Maris Mtwara ambacho ni Kampasi ya Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agostino Tanzania. Baadae mnamo mwaka 2012 - 2013 - Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Stella Maris Mtwara.Wakati akiwa Makamu wa Rais katika Chuo Kikuu Kishiriki Cha Stella Maris Mtwara alipata nyadhifa mbili ambazo ni Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agustino Tanzania na hatimaye kuwa Kiongozi wa Kitaifa ambapo alikuwa ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania. Kwa sasa ni Kiongozi wa Kisiasa katika Chama Cha Mapinduzi.